MBUNGE wa Mtama Nape Nnaye amesema kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mhe Samia Suluhu Hassan ni mfano wa Serikali sikivu  hasa kwa kutoa nafasi ya kutoa muda wa kufafanua masuala mbalimbali ya Wananchi.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa korosho kilichowakutanisha na Waziri Mkuu, Nape amesema, Wananchi wa Lindi wamepokea kwa mikono miwili na furaha uamuzi wa Rais Samia wa kuamua kuwatua wakulima wa korosho shilingi 110 baada ya maombi yao waliyowasilisha kama wawakilishi wa wananchi.

Nape amesema kuwa, Mamlaka ya mapato (TRA,) mkoani Lindi walitoa taarifa ya kuanza kukatwa kodi kwa wakulima wa mazao ya biashara wenye mapato yanayoanzia shilingi milioni nne na kuwataka wakulima hao kupeleka makisio ili waanze kukatwa kodi jambo lililozua taharuki kwa wakulima hasa wakorosho.

Amesema, licha ya kuwepo kwa makato mengi kwa zao la korosho, TRA wakaja na sheria ya kukata kodi zaidi kwa wakulima hao kwa sheria ambayo ni kandamizi ambayo Serikali haina budi kufuta na kuiondoa kabisa.

Kuhusu pembejeo za kilimo Nape amesema bado hazitoshelezi licha  ya Sensa ya kilimo kufanyika kwa wakulima hao.

Vilevile ameiomba Serikali kuharakisha malipo ya fedha kwa wakulima na ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa muda wa kwenda kukutana na wakulima na kufafanua kuhusu jambo hilo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe.Nape Nnaye alipokuw akizungumza nae jambo Bungeni hivi karibuni.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...