Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameitaka Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na kuendeleza mazungumzo ya mara kwa mara yatakayo wawezesha  kuepuka sintofahamu ambayo inaweza kutokea kwa kutokuzungumza kwao.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha watendaji wa Jumuiya hiyo pamoja na Mabalozi wa nchi za Jumuiya wanachama EAC walioko nchini Tanzania katika Makao Makuu ya EAC Mkoani Arusha kujadili masuala ya mtangamano pamoja na maamuzi yaliyofanywa na vikao vya ngazi ya juu.

Balozi Milamula amesema kama Wizara ya mambo ya nje watachukulia shughuli za Jumuiya na umuhimu wake kwa kuhakikisha mtengamano unakaa vizuri katika uchimi,biashara,siasa na masuala mingine mtambuka ili kuwezesha jamii kufahamu kinachoendelea katika Jumuiya hiyo na kuwa sehemu ya ushirikiano wa kijumuiya.

"Niiombe Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,wengi hawajui wanafikiri ni wafadhili wa nje ndiyo wanaofanya haya,huo ndio msisitizo wangu."Alisisitiza Balozi Liberata Mulamula.

Kwa upande wake Katibu mtendaji wa Jumuiya  hiyo,Peter Mathuki amesema kikao hicho kimelenga kuangalia mbiu ambazo zitatumika katika kuimarisha jumuiya hiyo kulingana na malengo tofauti yaliyopo katika kuboresha masuala ya kiuchumi na kubiashara.

"Kutokana na malengo tofauti tuliyonayo katika Jumuiya yetu tutaangalia njia bora ambazo zitatuwezesha kuboresha uchumi na biashara na kutatua vikwazo vilivyopo lakini kuimarisha Jumuiya."Alisema Peter Mathuk,Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kikao na Mabalozi wa  EAC

Naye Balozi wa Kenya nchini Tanzania,Dan Kazungu akizungumza kwa niaba ya Mabalozi wa Jumuiya hiyo amesema kuwa kama mabalozi wataunga mkono misingi,kazi na juhudi kuhakikisha Jumuiya inasimama imara kwani ushindi wa jimuiya hiyo ni ushindi wa Jumuiya yote ya Afrika Mashariki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walioko nchini Tanzania katika kikao kazi chao.
Katibu mtendaji wa Jumuiya  hiyo,Peter Mathuki akieleza malengo ya kikao kazi na namna watakavyoweza kutatua vikwazo vinavyowakabili katika Jumuiya hiyo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...