TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imewataka wawezeshaji wa ujaribishaji wa mwongozo wa kufundisha elimu stadi za maisha za afya ya uzazi ,VVU/Ukimwi na jinsia kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kuwa na uzalendo katika kuifanya kazi yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba katika ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa siku sita ambapo amewaeleza washiriki mafunzo waliyoyapata yawe chachu katika utaoji wa elimu ya afya ukiwemo maambukizi ya VVU , ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.

“Ningependa ifahamike kwa sasa Miongozo hii ipo kwenye majaribio , wawezeshaji wakati mnapofanya ujaribishaji mnapaswa kufuatilia na kupata mrejesho ya kipi kinahitajika katika kufanyiwa marekebisho’ amesema Dkt.Komba.

Ameongeza TET kwa kushirikiana na Shirika la UNESCO,TACAIDS,Maria Stops na shirika la Room to Read watafuatilia kwa karibu ujaribishaji wa miongozo hiyo katika halmashauri zote 13 zilizopanga kufikiwa.

Kwa upande Mmwakilishi kutoka wizara ya TAMISEMI Teresia amesema miongozo hiyo itasaidia katika kupunguza au kumaliza kabisa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kwa wahusika watakaopatiwa elimu hii ya stadi za maisha itasaidia wanafunzi kuweza kupambana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo wanafunzi wengi kushindwa kumaliza Shule .

Ameongeza kuwa TAMISEMI imefurahishwa na kuona walimu wengi wameweza kupata mafunzo hayo ambayo kwa vitendo na kuwa kila Shule itaweza kuwa na walimu wawili wawilii kwa Shule za Msingi na Sekondari na wataweza kufundisha stadi za maisha kwa wanafunzi.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku sita na kuwashirikisha jumla ya washiriki 46 wakiwemo Walimu ,maofisa kutoka TAMISEMI, Wakufunzi na wataalamu wa afya ambapo jumla ya walimu 1696 wa shule za Sekondari na Msingi wanatarajiwa kuwezeshwa kwenye mafunzo hayo kwenye halmashauri 13.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania  (TET), Dkt. Aneth Komba akitoa hutoba ya kufunga mafunzo hayo kwa wawezeshaji wa ujaribishaji mwongozo  wa kufundisha stadi maisha.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akiwa katika picha ya pamoja wakati wa kufunga mafunzo kwa wawezeshaji wa ujaribishaji mwongozo  wa kufundisha elimu stadi maisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...