Na Godfrey Andafiche

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (Bongo Flava) Faustina Mfinanga maarufu kama Nandy amewataka Wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuchangamkia fursa ya kujisajili na mtando wa TTCL ambao unawapa unafuu wa huduma za mawasiliano.

Nandy ameyasema hayo leo alipofanya ziara yake katika Ofisi za TTCL zilizopo Nyamagana jijini Mwanza akiwa ameambatana na Wasanii wenzake waliomsindikiza katika kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kupitia Tamasha la TTCL Nandy Festival 2021.

Akiwa Ofisini hapo ametoa shukrani za dhati kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania kwakuona umuhimu wa kuwezesha tamasha hilo linalolenga kuwapa burudani Mashabiki, wapenzi wa muziki na kuwarudisha nyumbani Wananchi ili waweze kutumia mtandano wao wa kizalendo wa TTCL.

“Natumia nafasi hii kuwakaribisha wakazi wote wa Mwanza kujiunga na TTCL kwa kujipatia laini bure na kujisajili bure pamoja na kulipia kiingilio cha tamasha letu kupitia T-Pesa” amesema Nandy 

Pia alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania na wanamwanza kiujumla kujiunga na mtandao wa  TTCL ili wanufaike na ofa ya WAKALISHE yenye Dakika 50 mitandao yote, SMS 50 na MB 150 bure kwa muda wa siku Saba.

TTCL Nandy Festival 2021 imesheheni wasanii maarufu ambao watatumbuiza leo jijini Mwanza katika viwanja vya Rock City Mall ambapo Wasanii hao ni pamoja na Fid Q, Baba Revo, Barnaba, Meja Kunta, Badest 47, Mabantu, Joh Makini, Stamina, Young Lunya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...