Mkurugenzi wa Msichana Initiative Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Madhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa Tasisi Tano zinazojiusisha na ulinzi wa Mtoto

Mkurugenzi wa Taifa wa Msaada wa Mtandaoni Kutoka Tasisi ya C Sema, Michael Marwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv.
TANZANIA inakadiriwa kuwa na kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni duniani, Kwawastani, karibu wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 na 37% ya wanawake wenye umri wa miaka 20-24 wameolewa ama wako kwenye mahusiano ya kinyumba kabla ya umri wa miaka 18.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi alipokuwa akizungumza na na Waandishi wa Habari katika mkutano ulioandaliwa na Azaki Tatu zinazojiusisha na ulinzi wa Mtoto.

Gyumi amesema kuwa wazazi wengi utumia mwanya wa sheria ya elimu kuwaozesha Watoto chini ya umri wa miaka 18 kwa madai kuwa awapo shuleni hivyo sheria ya ndoa inawaruhusu.

“Mwaka 2016, Msichana Initiative Organization ilifungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba kubatilisha vifungu vya 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa, 1971 kwa kuvunja haki ya msingi inayolindwa na katiba na hivyo kumnyima mtoto wa kike fursa kama vile haki ya elimu.

Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja za Msichana Initiative na kuamua kwamba vifungu hivyo ni batili na kinyume na katiba. Hata hivyo, mwaka 2017 serikali kupitia Mwanasheria Mkuu ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Mnamo Oktoba, 2019 Mahakama ya Rufaa iliridhia uamuzi huo wa Mahakama Kuu na kuiamrisha serikali kupitia bunge ifanye mabadiliko ya sheria husika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.” Amesem Gyumi

Gyumi amesema huu ulikuwa uamuzi muhimu sana kuhusu haki za msichana Tanzania na nafasi adhimu kuchochea haki na maendeleo ya msichana pande zote za Tanzania.

Gyumi ametaja kuwa Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa unapaswa kuchochea mabadiiliko ya Sheria ya Ndoa, 1971, (Kama ilivyorejewa mwaka 2009) hususani vifungu vya 13 na 17.

Aidha ametoa wito kwa serikali kuharakisha marekebisho ya Sheria ya Ndoa kwakuwa pasipo kufanya hivyo asilimia thelathini na moja (31%) ya wasichana wataendelea kuingia kwenye ndoa za utotoni kabla ya umri wa miaka 18 na asilimia tano (5%) kabla ya umri wa miaka 15.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa Kulingana na utafiti wa sasa, uwepo wa ndoa za utotoni ni mkubwa kwenye mikoa ya Shinyanga (59%), Tabora (58%), Mara (55%) na Dodoma (51%) 2 . Uwepo wa ndoa za utotoni ni mdogo Iringa (8%) na Dar es Salaam (17%).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taifa Msaada kwa mtandao kutoka Tasisi ya C Sema, Michael Marwa ametaja kuwa huduma ya Simu kwa Mtoto hupokea kesi 7 za ndoa za utotoni kila mwezi jambo ambalo limeulazimu uongozi wa Huduma hii kuungana na Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni (TECMN), ambao ni muungano wa asasi 35 zinazofanya kazi pamoja kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania hususani, kuongeza uelewa wa madhara ya ndoa za utotoni katika ngazi ya jamii na taifa.

Save the Children Utafiti uliofanywa na Save the Children umeonyesha kwamba elimu na makazi salama yasiyo na migogoro ni miongoni mwa masuala yanayosaidia kuwalinda wasichana dhidi ya ndoa za utotoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...