Na Gift Thadey, Babati
TIMU
10 za soka za Tarafa ya Mbungwe Wilayani Babati Mkoani Manayara,
zinatimua vumbi kwa ajili ya michuano ya Trump Cup inayofanyika kwenye
Kata ya Magugu.
Mdhamini
wa mashindano hayo Gabriel Lucas Nyange Trump amesema lengo la
mashindano hayo ni kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wa
eneo hilo.
Trump amesema vijana wa eneo hilo kipindi cha jioni wanashiriki michuano hiyo ambayo itasababisha umoja, upendo na mshikamano.
Dwani wa Kata ya Magugu, Filbert Modamba amemshukuru Trump kwa kuwezesha michuano hiyo ambayo ni chachu kwa vijana.
Modamba
amempongeza Gabriel Nyange Trump kwa kuanzisha mashindano hayo ya Trump
Cup ambayo yamesababisha hamasa kwa vijana kupenda michezo.
Mkuu
wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU wa Mkoa wa Manyara, Thomas Mbilinyi
anasema michuano hiyo itasaidia kupunguza uhalifu kwenye eneo hilo.
Mbilinyi
amesema wadau wengine wa michezo wamuige Gabriel Nyange katika
kuanzisha mashindano mbalimbali kwenye maeneo tofauti ya mkoa wa
Manyara.
"Wadau wengine
wa miji midogo ya Galapo, Mirerani, Orkesumet, Kibaya, Katesh na
kwingineko waige mfano huu kwa kuwakutanisha vijana pamoja kwenye
michezo," amesema Mbilinyi.
Mwenyekiti
wa mashindano hayo ya Trump Cup, Mohamed Kulanjiti amesema timu hizo 10
zimetokea kwenye Kata saba za Tarafa ya Mbungwe.
"Katika
timu hizo 10 kila kata imetoa timu moja na nyingine zimetoa timu mbili
hadi kufanikisha kuwepo kwa timu hizo zinazoshiriki Trump Cup," amesema
Kulanjiti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...