Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizindua rasmi show mpya "Bingwa" inayojumuisha vijana katika Sekta mbalimbali waliopatikana kupitia mitandao ya kijamii
Baadhi ya Washiriki Wa Show hiyo ya Bingwa inayoanza rasmi Julai 12,2021 na kufika tamati Septemba 25 mwaka huu itakayorushwa kupitia tv3 katika King'amuzi cha Startimes



Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

KAMPUNI ya Startimes  imewakutanisha vijana wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii kwenye Reality Show inayokwenda kwa jina "Bingwa".

Akizungumza na Michuzi Tv Mara baada ya kutambulisha rasmi Msimu wa Kwanza wa show hiyo Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema ni wakati wa watazamaji kuona Maisha halisi ya watu ambao wamekua wakijihusisha na vitu mbalimbali vya kiburudani kuanzia Filamu,Muziki, wajasiriamali pamoja na wanamitindo.

"Ni moja ya kipindi ambacho kitarushwa kupitia tv3  na Washiriki wataanza kukaa kwenye jumba la kifahari Julai 12 mwaka huu huku sehemu kubwa ya Washiriki ni Vijana ambao wanaonekana katika jamii na kujihusisha na vingi hasa vya kiburudani Kuna harmorapa Msanii wa Muziki, patrick kanumba na wengine wengi ambao tuliweza kuwapata kwa kupitia Mchakato wa majina yao kupendekezwa kwenye ukurasa wetu wa Instagram."

Aidha,Malisa ameeleza kuwa kupitia show hiyo watazamaji wataweza kujishindia zawadi kwa Msimu wote wa show hiyo na watazamaji wataweza kuwapigia kura Washiriki hao kwa kupitia Startimes on pamoja na Mshindi kuibuka na zawadi ya gari ambalo bado halijafahamika pamoja na pesa taslim Milioni kumi .

"Watazamaji wataweza kujishindia zawadi mbalimbali, hivyo kwa Sasa waendelee kuwapigia kura Washiriki ili tuweze kupata Washiriki 16 ambao wataingia kambini rasmi na kambi itachukua takribani siku 60 na zawadi mbalimbali zitatolewa kwa Washiriki wote huku Mshindi ataibuka na gari ambalo tutatolea ufafanuzi siku za usoni lakini kwa Sasa Mshindi atapewa milioni kumi za kitanzania."

Pia Malisa ameongeza kuwa show ya Bingwa itaonyeshwa kuanzia jumatatu Hadi jumamosi kuanzia saa 3 mpaka saa 4 kamili huku akiwasihi watazamaji kulipia visimbuzi  vyao.

Kwa upande wake Mzalishaji Mkuu wa show hiyo James Luvamda amesema  vijana wengi wanatumia  mitandao ya kijamii na wengi wamekuwa na ushawishi mkubwa Sana katika jamii.

"Hivyo tumeona tuwakutanisha wale ambao wanafanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii hasa hasa Instagram na pia Facebook wanaweza kunitumia mitandao ya kijamii vizuri na wakaweza kubadilisha Maisha yao ndio maana tumekuja na Bingwa ".

Pia Mzalishaji Mkuu ameeleza kuwa kupitia show hiyo itaweza kuleta mabadiliko na kuwapa nafasi watuamiaji wa mitandao ya kijamii kama chanzo Cha kujipatia ajira.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tafadhali tuwe tunapewa Email ya show ya Bingwa Ili Tuwe tunatuma maonii yetu huko Pia.

    Nashukuru.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...