Na Karama Kenyunko Michuzi TV 

MKURUGENZI wa mashtaka nchini (DPP) amewafutia shtaka la utakatishaji fedha  wakurugenzi wa kampuni ya kuagiza vinywaji vikali nchini, Bevco Limited na sasa wako huru kuomba dhamana.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni zoezi endelevu la DPP katika kupunguza msongamano wa mahabusu gerezani.

Mapema wakili wa serikali, Ester Martin alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Isaya kuwa leo Juni 24,2021 kesi hiyo ya uhujumu uchumi imekuja kwa ajili ya kuifanyia mabadiriko hati ya mashtaka kwa kuondoa shtaka moja la utakatishaji fedha na kuwasomea washtakiwa mashtaka yaliyobaki.

Katika kesi mpya washtakiwa wanakabiliwa na makosa 48. Lipo shtaka moja la kuongoza genge la uhalifu, mashtaka matano ya kushindwa kulipa kodi, mashtaka saba ya kughushi, mashtaka saba ya kutoa nyaraka za uongo, mashtaka 14 ya kukwepa kodi na shtaka moja la kusababisha hasara kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya Sh bilioni 1.6.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Melaine Philipe na Thierry Lefeuvre raia wa Ufaransa,  Joseph Rwegasila aliyekuwa Diwani wa a Makongo na Mwanasheria Ntemi Massanja.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Septemba Mosi mwaka 2017 hadi Septemba 2020

Washtakiwa wanadaiwa kwamba kati ya Oktoba mwaka 2017 hadi Juni mwaka 2020 jijini Dar es Salaam, waliisababishia TRA kupata hasara ya Sh 1,658,370,376.29.
 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julia 6, mwaka huu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...