Wafanyakazi wa 
Kituo cha Msaada kwa wanawake (WLAC) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali za mtaa pamoja na watendaji wa kata ya Mtoni iliyopo Tekeme Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya semina iliyotolewa na Kituo cha Msaada kwa wanawake (WLAC).
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mtoni, Anaklet Hayuka akipokea vitabu kutoka kwa Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Barcoal Deogratius vinahusiana na sheria ya Kazi na Ajira. Vitabu hivyo ni kwaajiri ya jamii kwa ujumla ili wajue sheria ya kazi na Ajira.
Mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu, George Mkangala akitoa mafunzo kwa watendaji wa serikali pamoja na viongozi wa serikali za mtaa wakati Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake(WLAC)walipofika kutoa mafunzo ya Sheria ya Kaiz na Ajira.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wakitoa maoni juu ya sheria ya kazi na Ajira mara baada ya wafanyakazi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake(WLAC)     kufika katika Kata ya Mtoni iliyopo wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

KITUO Cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake(WLAC) watoa mafunzo kwa viongozi wa serikali ya mtaa na pamoja na watendaji wa kata hiyo.

Akizungmza wakati wa kutoa mafunzo ya nayotolewa na Kituo cha Msaada kwa wanawake (WLAC), Mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu, George Mkangala amesema kuwa kila mfanyakazi ana haki ya kupata likizo ikiwemwo likizo ya mwaka.

Mkangala amesema kuwa sheria imebanisha aina tofauti ya likizo zikiwemo likizo za uzazi, likizo ya ugonjwa na likizo nyingine.

Akitoa mafunzo hayo Mkangala alikazi sehemu ya likizo ya Ugonjwa amesema kuwa likizo hiyo kwa kila mfanyakazi ana haki ya kupata angalau siku 126 katika mzunguko wa likizo ndani ya miaka mitatu au miezi 36.

Amefafanua kuwa likizo ya siku 63 za kwanza mfanyakazi atalipwa mshahara mzima lakini siku 63 zinazofata mfanyakazi atalipwa nusu mshahara.

Hata hivyo ametoa mkazo kuwa likizo hiyo itatolewa endapo mfanyakazi atawasilisha cheti cha matibabu kilichotolewa na tabibu aliyesajiliwa na kukubali bila sababu za msingi.

Licha ya hivyo ametoa ufafanuzi juu ya likizo ya uzazi kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) cha sheria na mahusiano kazini 2004 amesema kuwa Mjamzito atatakiwa kutoa taarifa ya kuwa atakuwa na likizo ya uzazi kabla miezi mitatu ya tarehe ya kujifungua na notisi hiyo itatakiwa kuambatana na cheti cha kitabibu.

"Kwa upande wa wanaume nitoe angalizo kutumia likizo ya uzazi kama lengo la likizo hiyo linavyoitaka." Amesema Mkangala

Kwa upande wa Afisa Afya wa Kata ya Mtoni, Helena Helman ameomba sheria ya  kazi na ajira ifanyiwe marekebisho kwani inapotungwa walilenga kwa watu wanaojifungua watoto mmoja au wawili tuu lakini kwa sasa inaonesha mtu anaweza kujifungua watoto zaidi ya wawili.

"Juzi kati tumesikia mama mmoja amejifungua watoto 10 je, huyu sheria ya ajira na kazi, kupitia kifung cha sheria ya likizo ya mfanyakazi atapata likizo ya siku ngapi?, ikiwa likizo ya mtoto mmoja ni siku 84?" Alihoji Helena.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Mtoni, Anaklet Hayuka amewashukuru Kituo wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) kwa kuichagua kata ya Mtoni kwa kutoa mafunzo hayo.

Mafunzo ya kuifahamu sheria za kazi na ajira zinazotolewa na Kituo wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) yanasaidi kupata maoni ya jamii juu ya masuala ya kazi pamoja na kusaidia baadhi ya sheria ziweze kufanyiwa marekebisho.

Kituo cha Msaada kwa wanawake (WLAC) pia walitoa Vitabu kwaajili ya kuwapa watu wengine na kuwafundishia watu wengine endapo wakipeleka mashtaka kwa kwani wao ndio huonana na wananchi wengi zaidi pale zinapotokea changamoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...