Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omari Juma Kipanga amesema kwa Serikali katika mkakati ambao utahakikisha wanafunzi wanaopata ujauzito wanarudi kuendelea na masomo yao baada ya kujifungua.

Akizungumza leo Juni 24,2021, wakati wa kongamano la wadau na wachangiaji wa elimu liliofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (DSM) likiwa na lengo kujadili na kuweka mikakati ya pamoja itakayowezesha kuzitatua changamoto zinazoikabili Sekta ya elimu nchini, Kipanga amesema suala la kupata elimu ni haki ya kila mtanzania.

"Suala la kupata elimu ni haki kila mtanzania, hivyo utaratibu utawekwa ili kuhakikisha waliopata ujauzito wanarejea kuendelea na msomo.Pamoja na jitihada za kukarabati na kujenga miundombinu mbalimbali lakini pia serikali imeweka nguvu kuboresha vyuo vya ualimu ili viweze kuzalisha walimu watakoendana na kasi ya Teknolojia."Amesema Kipanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bahati Geuzye amesema zaidi ya Sh.Bilioni 9.1 zilitumika kufadhili miradi 96 ya elimu katika shule 88 na taasisi moja ya sayansi na teknolojia kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

"Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya shule 116 zinanufaika na miradi 123 inayogharamia jumla ya shilingi Bilioni 9.4.Aidha jukumu la msingi la mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA ni kuongeza jitihada za serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na upatikanaji wake wa usawa," Amesema.Ameongeza kupitia mfumo huo taasisi za elimu kuanzia ngazi ya shule za msing, Sekondari, vyuo vya kati na vyuo vya Elimu ya juu vinapata fursa ya kufadhiliwa miradi inayolenga kuboresha mazingira na kujifunza na kujifunzia.Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Omari Juma Kipanga akizungumza na waaandishi wa habari leo wakati wa kongamano la wadau na wachangiaji wa elimu liliofanyika katika ukimbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (DSM) (Picha na Emmanuel Massaka, Michuzi TV)Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi.Bahati Geuzye akizungumza katika kongamano la wadau na wachangiaji wa elimu liliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (DSM) lengo kujadili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...