NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO
Akitoa taarifa kwenye kikao cha kamati ya lishe ya wilaya ya Namtumbo mratibu wa kamati ya lishe Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Sosteneth Mumba alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja 2020/2021 Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imewabaini watoto 35 wenye utapiamlo mkali
Mumba alidai watoto 35 kuanzia miezi sita na chini ya miaka mitano waliobainika walitokana na kuwapima watoto 10,689 katika kata 21 na vijiji 66.ambao kati ya hao 35 ndio waligundulika na utapiamlo mkali katika Halmashauri ya wilaya Namtumbo.
Mtendaji wa kata ya Rwinga bwana Mario Mwageni alilalamikia ugumu wa ukusanyaji taarifa za lishe katika kata yake akidai kata yake haina watendaji wa vijiji kutokana na kata hiyo kuwa sehemu ya mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo hivyo kuwatumia wahudumu ambao sio waajiriwa wa serikali wanafanya kazi hizo za kukusanya taarifa za lishe watakavyo wao .
Aidha bwana Mwageni aliongeza kuwa wahudumu ngazi za vijiji wanapaswa kutoa elimu kupitia mikutano ya hadhara ya vijjji kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji ili kuelimisha jamii iweze kuelemika katika swala la lishe na kuepukana na utapiamlo.
Mwenyekiti wa kamati ya lishe wilaya ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Namtumbo Julius Kenneth Ningu aliwataka watendaji wa kata,vijiji kwa kushirikiana na wahudumu wa afya ngazi za vijiji kutoa taarifa zenye uhalisia kuhusu hali ya lishe katika mazingira yao .
Ningu pamoja na mambo mengine aliwataka pia watendaji kupitia mikutano ya vijiji kutumia muda wao kutoa elimu ya lishe kwenye vikao vyao kwa kuwaalika wataalamu ili kuwaelimisha wananchi kuzingatia maswala ya lishe kikamilifu ili kupunguza watoto wapatao utapiamlo katika wilaya ya Namtumbo .
Kikao cha kamati ya lishe wilaya kimefanyika kwa lengo la kutoa taarifa ya hali ya lishe katika wilaya ya Namtumbo ambapo kwa kipindi cha mwaka mmoja 2020/2021 watoto 35 kati ya 10,689 wamegundulika kuwa na utapiamlo mkali wilayani Namtumbo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...