Na Karama Kenyunko - Michuzi TV
ALIYEKUWA askari polisi, F. 6763 Koplo Deodatus Massare (37), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilogramu 1.04.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Luambano imedai, June 19,2021 huko eneo la Bunju Beach ndani ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiww alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilogramu 1.04.
Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza hiyo kwa kuwa ni kesi ya uhujumu uchumi.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 29,2021 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa mshtakiwa amerudishwa rumande.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...