CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)kimesema kinawakaribisha wahitimu wenye sifa wa kidato cha sita, na Astashahada kujiunga nacho katika programu mbalimbali kwani watakuwa wahitimu bora kutokana na mifumo thabiti ya usomaji na ufundishaji ikiwemo ya njia ya mitandao iliyopo chuoni hapo.
Hivyo chuo hicho kimewakaribisha wanafunzi kujiunga na kozi mbalimbali ambapo wanafunzi watakaojiunga watapata faida ya kusoma na kujifunza kwa vitendo kwa kutumia miundo mbinu bora .
Akizungumza leo Julai 29,2021 kwenye Maonesho ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Mahusiano Masoko wa chuo hicho Dk.Mohamed Maguo amesema watakaojiunga na programu mbalimbali katika chuo hicho watapata faida katika kusoma kwa kujifunza kwa vitendo kwa kutumia miundo mbinu bora ikiwemo kupitia tehama .
"Kuna matawi ya OUT kwa kila mkoa ambapo mwanafunzi hana haja ya kuja makao makuu anasoma na kujifunza huko alipo tunawalimu waliobobea na mifumo bora ya ufundishaji hasa hasa ya mitandaoni ," amesema Dk.Maguo na kuongeza kwa kutumia nyenzo hizo wahitimu katika chuo hicho ni lazima watakuwa wahitimu bora.
Wakati huo huo amesema Chuo hicho kinawakaribisha wanafunzi wa kidato cha sita na ngazi zingine waliopungukiwa sifa ya kujiunga na Shahada ya kwanza kwani waliokosa sifa wataweza kupata kozi inayowawezesha kujiunga,hivyo watasoma mwaka mmoja ndipo watajiunga na shahada hiyo katika chuo chochote kilicho nchini au nje ya nchi.
Amesisitiza kwa wahitimu wa kidato cha nne wasio na sifa wanapewa nafasi kujiunga na OUT kwa kupitia kozi hiyo na watapomaliza watakuwa na uwezo kusoma ngazi ya cheti katika chuo chochote au nje.
Amefafanua mhitimu wa kidato cha sita aliyepata daraja la tatu la pointi 14 atalazimika kusoma kozi hiyo(Foundation Course) kwa mwaka mmoja ndipo kuendelea na masomo ya Shahada ya kwanza huku wale waliomaliza Astashahada waliopata chini ufaulu wa G.P.A ya 3.0 watasoma kozi hiyo.Pia kozi hiyo ni pamoja na waliomaliza ngazi ya cheti NTA level 5 waliosoma miaka mitatu wataingizwa kwenye kozi hiyo .
Ameeleza kwamba chuo hicho kilianzishwa mwaka 1992 kwa sheria Na17 ya Bunge inayokipa maelekezo ya kutoa elimu ya Juu kwa njia huria na masafa na kusisitiza bado kuna nafasi nyingi za kujiunga pasipo gharama yoyote ya maombi.
Ameongeza wahitimu wa kidato cha sita,Astashahada, cheti ambao waliokosa sifa ya kujiunga shahada ya kwanza watalipia ada ya Sh 720,000 kwa kozi ya mwaka mmoja itakayomwezesha kujiunga Shahada ya kwanza (Foundation Course) huku waliomaliza cheti kwa Levi hiyo watalipa sh milioni 2.4.
Dk.Maguo amesema kwa mwaka wa masomo 2020/21 waliweza kudahili wanafunzi 16,000 mpaka 20,000 na kwamba chuo hicho kina wanafunzi 60,000 huku wanaosoma ana kwa ana wahitimu ni 20,000 na 40,000 ni wale wanaoahirisha mwaka wa masomo ambapo wamejipanga kudahili wanafunzi zaidi kwa mwaka huu.
Katika hatua nyingine ,Dk.Maguo amesema OUT kina program zaidi ya 100 kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya Uzamivu pamoja na kozi takribani 1,000.Amesema wanafunzi watakaosoma OUT watapata fursa ya kujisomea kupitia maktaba ya mtandao kwa ruhusa kuingia pale anapolipia ada ,ratiba ya mafuzo ya ana kwa ana kwa wanafunzi wenye vikwazo watakutana na walimu wao popote walipo.
Pia amesema wanafunzi wa chuo hicho wameunda makundi ya mtandaoni ya majadiliano ya programu mbalimbali (Whatsapp discussion) ambapo kuna viongozi ndani yake hujadiliana masomo na pale panatokea changamoto huwasiliana na walimu wao kuzitatua.
Dkt. Maguo alisema makundi hayo yatawaunganisha wanafunzi wanaosoma OUT kujifunza mtandaoni na limepewa jina la WhatsApp ni kimbweta kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Amesema wanafunzi wa Chuo hicho utumiaji wa What's App kama Kimbwette cha kufanyia majadilianoya masomo yao itasaidia kwa kuwa itachea kuwaweka sawa kwa hakika kila uchao ubunifu katika TEHAMA unaendelea kusaidia sana katika ElimubHuria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...