Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Mchora Katuni maarufu hapa nchini na Mtangazaji, Masoud Kipanya ameeleza sababu ya kifo cha Mtoto wake, Malcom kilichotokea jana Julai 28, 2021 wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi baada ya afya yake kubadilika ghafla akiwa na Mama yake mzazi nyumbani.

Akizungumza baada ya kumpunzisha marehemu Malcom katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam, Masoud Kipanya amesema siku chache kabla ya umauti, Malcom alisumbuliwa na homa, amesema walipoona hali hiyo waliita Muuguzi aliyefika nyumbani mara kwa mara kwa ajili ya matibabu kutokana na hali yake.

“Enzi za uhai wake maisha yake yote yalikuwa ni Dawa tu, sisi Walezi wake tulihakikisha maradhi hayamfikii mara kwa mara na tulijitahidi hapatwi na maradhi yoyote”, amesema Masoud Kipanya.

Amesema siku ya jana baada ya hali yake kubadilika walimpigia simu Daktari Elisha Osati na kumuelezea hali ya Malcom ambapo waliambiwa apelekwe Hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Nilimpigia Dkt. Osati kuhusu afya ya Malcom, lakini Daktari aliniambia tumpeleke Hospitali moja ipo Upanga, sisi tulimpeleka na huwa tunatumia Gari maalum la Wagonjwa (Ambulance). Walimpiga X-Ray baadae waligundua upande mmoja wa Mapafu yake umejaa Maji”.

Masoud amesema waliruhusiwa kurudi nyumbani na baadae alipigiwa Simu na Mke wake (Mama Malcom) akieleza kuwa hali ya mgonjwa imebadilika ghafla. Baadae marehemu Malcom alikimbizwa Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi baada ya hali hiyo.

“Ambulance ilipofika Muhimbili, Daktari aliingia ndani ya hiyo Ambulance na kusema kuwa Malcom hatunaye tena duniani, lakini kabla ya kufika Malcom aliwekewa Oxygen kwa ajili ya msaada wa kupumua. Kifo chake kimetokea akikimbizwa Hospitali ya Muhimbili”, ameeleza Kipanya.

Marehemu Malcom amefariki dunia hapo jana (Julai 28, 2021) baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Misuli kutokuweza kufanya kazi.

Ina Lilah Waina ilayhi Raji'un, Hakika Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...