Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

NAIBU Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema mamlaka ya maji  safi na usafi wa mazingira DAWASA imepiga hatua kubwa katika usimamizi wa miradi ya maji nchini ikiwemo matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika Mamlaka hiyo kwa kuwekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 17.8 katika Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua kero ya Maji kwa Wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ziara hiyo, Naibu Waziri, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapongeza DAWASA kwa kujituma kutekeleza Miradi hiyo ya kimkakati ili kutatua kero ya Maji katika sehemu mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Pia amepongeza Watumishi, Wasimamizi wa Miradi yote ya DAWASA wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Cyprian Luhemeja katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi hiyo takribani 27 sehemu mbalimbali ya Dar es Salaam na Pwani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA, Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi utakaosaidia kuondoa kero ya Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu wanalaza mabomba kwa umbali wa Kilometa 59  katika Mitambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.

Amesema pia mradi huo utatatua kero ya Maji katika Bandari Kavu ya Kwara na kwenye Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR Kwara, amesema Lita 9,300,000 za Maji zitatumika kwa siku baada ya kukamilika Mradi huo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhwan Kikwete amesema ujio wa Naibu Waziri wa Maji katika Maeneo hayo itasidia katika utekelezaji wa Miradi hiyo ya Maji na kuondoa kero kwa Wananchi wake.
.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi kuhusu ulazaji wa Bomba za inchi 10 zinazolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka Mboga yenye kilometa 58.9 kwenye Mradi wa Chalinze- Mboga unaotekelezwa na DAWASA. Wa kwanza kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi
Muonekano wa Bomba la inchi 16 linalolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka Mboga litakalokuwa na kilometa 58.9 
Kazi ikiendelea
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi kuhusu ulazaji wa Bomba unavyopita kwenye ramani kuanzia Ruvu Juu mpaka Mboga kilichopo Wilaya ya Bagamoyo  wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akikagua mradi wa ulazaji wa mabomba ya inchi 16 katika eneo la Kitongoji cha Mbala kilichopo Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara yake ya kukagua Miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Kazi ikiendelea 
Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu mradi wa kujenga pampu ya kusukuma maji katika Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara ya naibu Waziri wa maji alipotembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu ujenzi wa pampu ya maji ya Msoga wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi  akiendelea na Ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ujenzi wa pampu ya maji ya Msoga kuhusu kuridhishwa na miradi inayotekelezwa na DAWASA wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Shirika hilo.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na DAWASA wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna wanavyosimamia miradi hasa ya maji ili kuondoa hadha kwa wakazi wa Chalinze ambao wanachangamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi alipokuwa anatembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipata ufafanuzi kutoka kwa kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi kuhusu ulazaji wa mabomba ya inchi 12 katika Kijiji cha Mazizi yanayotoka Wami yatakayoweza kuhudumia maeneo ya Chalinze, Pingo, Pera, Msoga, Bwilingu, Msata, Kihangaiko, na Ubenazimozi.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi kuhusu usimamiaji mzuri wa miradi ili kumalizika kwa wakati kwa ajili ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya Chalinze wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani  wakiendelea kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipata kutoka kwa Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi kuhusu ujenzi wa pampu za kusukimia maji wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji leo.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayefanya ujenzi ndani ya Wami kuendana na muda uliopo kwenye mkataba.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...