Na Mwandishi Wetu

DROO ya Promosheni ya mwisho ya SportPesa iliyopewa jina la Mshiko Deilee imefanyika leo na Joshua Sukambi, 24 kutoka Kigamboni jijini Dar es Salaam amejishindia kitita cha Sh 15.8Mil.

Promosheni hiyo imefikia tamati leo baada ya kuchezeshwa kwa siku 30 ikishirikisha kampuni za Mitandao ya Simu ya TigoPesa, MPesa na Airtel Money.

Akizungumzia baada ya kupigiwa Simu na Wachezesha Droo hiyo, Joshua alianza kwa kushukuru baada ya ushindi huo na kusema kuwa “Najisikia freshi kabisa baada ya ushindi wangu, mimi ni kijana ninajishughulisha na biashara ya udereva wa bodaboda”.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas, amempongeza mshindi huyo na wengine waliokuwa wakishinda droo ndogo za siku na wiki akiamini pesa walizokuwa wanashinda zitabadili maisha yao.

“Leo tumefikia tamati ya promosheni yetu ya Mshiko Deilee yenye lengo la kuwatunza wachezaji wetu kila siku na wiki walikuwa wakipata zawadi na kutokana promosheni tuliyokuwa tunaiendelesha kwa kushirikiana na TigoPesa, Airtel Money na MPesa.

“Ninaamini Sh 15.8Mil inakwenda kubadilisha maisha ya Joshua ambaye ni dereva wa Bodaboda ambayo kama siyo yake, basi ninaamini atanunua yake na kuimiliki ili kusaidia familia yake.

“Kwa washindi wetu wa Sh 100, 000, 000 wa kila wiki tunaamini zitawasaidia washindi wetu kuboresha ama kuanzisha biashara kwa mtaji huo ikiwa wanajishughulisha.

“Tunawaomba Watanzania wengine waendelee kucheza na SportPesa ili na wao wajishindie pesa zitakazobadili maisha yao kama ilivyokuwa kwa huyu kijana aliyejishia Sh 15.8Mil ambazo ninaamini maisha yake yatabadilika kwake na ndugu waliomzunguka,”anesema Tarimba.

Kwa upande wa Muwakilishi kutoka Tigo, Fabian Felician ambaye ni Ofisa Huduma wa Kitengo cha TigoPesa  alisema kuwa “Tunafurahia ushirikiano mzuri na SportPesa katika kuwezesha droo hii ambayo washindi wa kila siku, wiki na huyu wa mwisho, hivyo tunashukuru kwa kutuamini.

Meneja Biashara wa Airtel Money, Aggrey Charles alisema kuwa “Tunafurahia ushirikiano mzuri kati yetu na SportPesa ambao walituamini na kufanya kazi kwa pamoja na kumpata mshindi wa mwisho, hivyo tunawaomba wateja wetu kufanya mihamala yao kupitia Airtel Money.

Naye Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga amesema kuwa “Tunawapongeza washindi wote kutoka SportPesa pamoja na huyu tuliyechezesha droo kubwa ya mwisho na kupatikana mshindi, pia niwapongeze SportPesa kwa kuchezesha droo yao kwa uwazi tukishirikiana na bodi hiyo.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa droo ya Promosheni ya mwisho ya SportPesa iliyopewa jina la Mshiko Deilee imefanyika leo na Joshua Sukambi, 24 kutoka Kigamboni jijini Dar es Salaam amejishindia kitita cha Sh 15.8Mil.
Promosheni hiyo imefikia tamati leo baada ya kuchezeshwa kwa siku 30 ikishirikisha kampuni za Mitandao ya Simu ya TigoPesa, MPesa na Airtel Money.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas katika Picha ya pamoja na Wachezesha droo hiyo, Eric Omondi na Frank Charles wa Sportpesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...