MTENDAJI Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt.Mussa Budeba , ameipongeza Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na wadau wengine walio katika Banda la Wizara hiyo kwa namna wanavyoendelea kuwahudumia  wananchi  na wadau wengine katika Maonesho ya 45 ya Biashara maarufu Kwa jina la Sabasaba  yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

Dkt.Budeba aliweza kutembelea mabanda mbalimbali ndani ya Banda la Wizara ya Madini.

Akiwa katika Banda la GST Dkt.Budeba alipata fursa ya kuona namna wataalam wa GST wanavyoendelea kuwahudumia wadau mbalimbali waliotembelea banda hilo.

Akizungumza na wadau waliofika katika Banda la GST Dkt.Budeba aliwapongeza kwa kutembelea banda la GST ili kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu utafutaji wa madini na huduma zitolewazo na GST kwa ujumla. Vilevile, aliwaalika wadau mbalimbali kutembelea banda la GST ili kufahamishwa madini yanayopatikana nchini Tanzania.  Aidha, aliwaalika wadau mbalimbali kuitumia GST ili kuongeza tija na uzalishaji katika shughuli  zao za utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji madini.

Maonesho haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 5/7/2021.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...