Na Karama Kenyunko Michuzi TV
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
amevitaka vyombo vya habari nchini, kutenga muda wa kutosha wa kurusha
na kutangaza taarifa za hali ya hewa ili wananchi wazipate kwa wakati na
kuzitumia kwa ufani.
Dkt.
Tulia ameyasema hayo leo Julai 10,2021 wakati wa ziara yake fupi katika
Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) zilizopo Ubungo
jijini Dar es Salaam.
Amesema,
taarifa za hali ya hewa ni muhimu sana kwa jamii nzima lakini katika
vyombo vya habari hapa nchini, taarifa hizi zmekuwa zikitolewa kwa
ujumla na kwa ufupi, kitu ambacho kinaweza kuathiri matumizi yake.
“Nitoe
wito kwa vyombo vya habari kuangalia namna ambavyo watakuwa wanazitumia
taarifa kutoka TMA na kuzitoa mara kwa mara ili kutusaidia sisi
wananchi kujiandaa na kufanya maamuzi sahihi katika mipango yetu,
tuangalie kama vyombo vingine vya habari vya mataifa ya nje, ukifungua
kila wakati unaangalia hali ya hewa” Amesema Dkt. Tulia
Pia
Dkt. Tulia ametoa wito kwa wananchi kuitembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania ili kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna
taarifa za hali ya hewa zinavyochakatwa kitaalamu hadi kumfikia
mtumiaji.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo
ya namna uchambuzi wa hali ya hewa unavyofanyika kwa njia ya modeli za
kimahesabu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakati
alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar
es Salaam.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akijionea hindi
utabiri wa hali ua hewa kila siku unavyorekodiwa katika studio za TMA
kwa ajili ya kuruka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati
alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar
es Salaam.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Tulia Ackson akipata maelezo ya
namna utabiri wa hali ya hewa unavyoandaliwa kuanzia ngazi za awali
kutoka kwa Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri, TMA, Samwel Mbuya wakati
alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar
es Salaam.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo
ya namna taarifa za hali ya hewa za muda mrefu zinavyohifadhiwa kwa
ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya kimkakati
kutoka kwa Meneja wa Klimatolojia, TMA, Dkt. Hashim Ng'ongolo wakati
alipotembelea ofisi za TMA, Makao Makuu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...