SHIRIKA la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP) leo Julai 29,2021 limepokea mchango wa tani za 36 za tende zenye thamani ya Dola za Kimarakeni 88,437 kutoka Ufalme ya Saudi Arabia kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaoishi mikoa ya Kusini-Magharibi mwa Tanzania.

Shehena hiyo ya tende itakuwa nyongeza kwa msaada wa chakula unaotolewa kila mwezi kwa zaidi ya watu 50,000 wakiwemo wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, watoto wenye umri chini ya miaka mitano na makundi mengine ya watu wanaoishi katika mazingira magumu katika kambi za Mtendeli, Nduta na Nyarugusu katika mkoa wa Kigoma. 

Taarifa iliyolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa mchango mchango huo umekuja kipindi ambacho WFP ina ombwe katika ufadhili ambao imepelekea utoaji wa chakula kufikia asilimia 68 tu ya msaada wa chakula unaosambazwa kwa wakimbizi nchini Tanzania.

"WFP inakishukuru Kituo cha Msaada wa Binadamu na Usaidizi cha Mfalme Salman kwa msaada wake endelevu. Tunafurahi sana kwamba Falme ya Saudi Arabia bado ni mmoja wa wafadhili wetu tunaowathamini nchini Tanzania, wanaoisaidia WFP kuwafikia watu wanaoishi katika mazingira magumu zaidi wanaohitaji msaada wa chakula,"amesema Mkurugenzi na Mwakilishi wa WFP Tanzania Sarah Gordon-Gibson katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika Ubalozi wa Saudi Arabia jijini Dar es Salaam.

Wakimbizi wanaitegemea WFP pekee yake kukidhi mahitaji yao ya chakula. Wanapokea kikapu cha chakula chenye mchanganyiko wa vyakula mbalimbali ukiwemo unga maalum uliochanganywa soya na mahindi, kunde, chumvi, mafuta yanayotokana na mimea na unga wa mahindi uliotiwa virutubisho. Ugawaji wa tende hizi utafanyika mwezi huu na utawanufaisha walengwa zaidi ya 50,000 na kuwapatia virutubisho wanavyohitaji sana.

Aidha hivi sasa WFP inasaidia zaidi ya wakimbizi 235,000 kutoka Burundi na Kongo waliopo katika makambi ya Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu mkoani Kigoma. Kati ya sasa na mwezi Juni mwaka 2022, WFP ina upungufu wa fedha wa takriban Dola za Kimarekani milioni 29.6 kwa ajili ya shughuli zake zinazohusiana na wakimbizi.


Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa ni Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2020. Sisi ni Shirika la Kibinadamu kubwa zaidi duniani, tunaookoa maisha wakati wa maafa na kwa kutumia msaada wa chakula tunajenga njia ya kuelekea upatakanaji wa amani, utulivu na ustawi kwa watu walioathirika na migogoro, maafa na madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...