Na: Abel Paul - Jeshi la Polisi Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP- Justine Masejo akiongea na waandishi wa habari leo amesema Tarehe 08.07.2021 muda wa 07:00 mchana huko maeneo ya Sombetini katika Jiji la Arusha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha lilimkamata na linaendelea kumhoji mganga wa kienyeji (jina limehifadhiwa) mkazi wa Sombetini jijini Arusha kwa tuhuma za kumshawishi mtuhumiwa wa tukio la ukatili dhidi ya Mtoto lililotokea tarehe 06 Julai mwaka huu eneo la Burka.

Amesema kuwa  tarehe 08 Julai mwaka huu tulitoa taarifa ya mtoto wa kiume mwenye miaka (4) ambaye alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na kutekelezwa katika eneo la Burka.

Kammda masejo amewaambia waandishi wa habari kuwa Katika mahojiano ya kina na mganga huyo wa kienyeji mkazi wa sombetini ambaye amekiri kumshawishi mtuhumiwa huyo aliyemfanyia ukatili mtoto wa miaka minne (04) ambapo alimshawishi kwamba ukifanya kitendo hicho kitamsaidia katika kesi zake pamoja na utajiri katika biashara.

ACP Masejo ameendelea kusemea Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha  linaendelea na Upelelezi pindi utakapokamilika Jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua za kisheria.

Katika tukio jingine kamanda Masejo amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia  ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania katika wilaya ya Monduli kwa tuhuma ya mauaji ya LAISI S/O LEMOMO (26) Mfugaji mkazi wa kijiji cha Lashaine wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.

ACP- Masejo amesemea Tukio lililotokea tarehe 12.07.2021 muda wa 10:00 Jioni huko katika kijiji cha Lashaine wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha, aidha katika kubaini undani wa tukio hilo timu ya makachero imefika eneo la tukio na inaendelea uchunguzi wa tukio hilo na pindi Upelelezi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa kamilika itatolewa.

Kamanda masejo ametoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za waganga wa kienyeji wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu ikiwa ni pamoja na kuwashawishi  watu  kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya kina mama na watoto,kwamba wakifanya hivyo watafanikiwa katika mambo yao mbalimbali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP- Justine Masejo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...