NA FARIDA SAIDY,MORGORO.
Jamii
imetakiwa kutumia nishati mbadala ili kutunza mizingira kwa kupanda
miti kufuatia kuwepo kwa uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli
za kibinadamu ikiwemo kilimo cha kuhama hama, kuchoma mkaa, na ufugaji
usiozingatia utaalam, ambapo hali hiyo imepelekea kuwepo kwa majanga ya
asili yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Rai
hiyo imetolewa na Msimamizi wa kampeni ya KESHO TUTACHELEWA Elibarick
Simon yenye lengo la kuhamasisha upandaji wa miti na utunzaji wa
mazingira hususani kwa vijana, inayosimamiwa na shirika lisilo la
kiserikali la Raleigh Tanzania.
Akizungumza kwenye
mkutano uliowakutanisha vijana kutoka Raleigh Tanzania walioshiriki
katika kampeni tofauti za uhamasishaji utunzaji wa mazingira hapa
nchini Elibarick Simon amesema shirika hilo kwa kushirikiana na
serikali imeweza kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwenye jamii.’
Kwa
upande wake mwakilishi kutoka wakala wa huduma za misitu nchini
Christopher Assenga amesema TFS inaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali wakiwemo Raleigh Tanzania katika upandaji wa miti ili kuweza
kurudisha uoto wa asili ambao umeharibiwa katika maeneo mbalimbali hapa
nchini.
Aidha amewataka vijana kushiriki katika
kampeni mbalimbali za upandaji miti hususani katika vyanzo vya maji
hali itakayosaidia kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama katika
maeneo mjini na vijijini hapa nchini.
Nae kiongozi
wa maradi wa “Kesho Tutachelewa” Saidi Swalehe amesema mpaka sasa
Raleigh Tanzania imepanda miti zaidi ya 85,394 ndani ya mikoa sita na
kuwafikia vijana 9,345 ambao walifanikisha zoezi la upandaji miti hiyo
katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Pia ameongeza
kuwa kupitia matamasha ambayo yalikuwa yanaendeshwa na Raleigh Tanzania
wameweza kuwafikia zaidi ya watu 2, 000 wakiwemo wanawake ambao
wamekuwa waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabia nchi yatokanayo na
uharibifu wa mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...