Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wananchi
wa kijiji na kata ya Lupanga,wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.Wamesema
wamekuwa wakilazimika kuficha maiti,kuzuia matangazo na kujizuia kulia
unapotokea msiba jioni au mchana majumbani mwao ili kuepuka ada ya
kulaza maiti mochwari inayofika zaidi ya elfu 50,000
Wananchi
wa kijiji hicho wameeleza changamoto hiyo katika mkutano wao na mbunge
wa jimbo hilo Joseph Kamonga alipofika katika kijiji hicho ikiwa ni
ziara yake anayoedelea kila kijiji ili kupata changamoto na kuzifanyia
kazi huku akitoa mrejesho kwa wananchi juu utekelezaji wa baadhi ya
changamoto zao za awali mara baada ya kuzifikisha katika halamashauri na
vikao vya bunge
Zebedayo
Mgaya ni mmoja wa wakazi wa kijiji hicho aliyeeleza changamoto hiyo
huku akibainisha kuwa amewahi kufiwa hivi karibuni na ndugu yake na
kulazimika kukaa kimya na maiti nyumbani kwake akihofia kutangaza kwa
kuwa uongozi wa kijiji hicho ungemtaka kufikisha mwili wa marehemu
mochwari iliyopo umbali wa zaidi ya KM 10 kutoka kwenye kijiji hicho
huku ghalama za usafirishaji pekee zikiwa ni shilingi elfu 40 mpaka 50
"Ghalama
za kusafirisha mwili kutoka hapa mpaka mochwari iliyopo Mlangali ni
zaidi ya KM 10 na ghalama zake ni elfu 50 mpaka 50 na sijui kwanini
ghalama ya kusafirisha maiti ni kubwa kuliko kusafirisha
mahindi.Nashauri kama Mochwari ni mradi mzuri kwa wizara ya afya au
halmashauri basi wajenge kila kijiji mahali ambapo mtu anaweza kufikisha
maiti na kurudisha nyumbani"alisema Zebedayo Mgaya
Aidha
wananchi wa kijiji hicho wamesema wamekuwa na hofu wanapopata msiba na
kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji kwa kuwa imekuwa ikiwalazimu
kufikisha maiti katika mochwari kutokana na kuto ruhusiwa kulala na
maiti huku wengi wao wakiwa hawana ada ya mochwari kwa wakati huo.
"Tumekuwa
na hofu kubwa mtu akifa jioni,watu huwa hawatoi yowe na inapofika siku
ya pili tunatoa taarifa ili ionekane mtu amekufa siku leo kumbe amekufa
jana ili tu kukwepa ghalama ya mochwari"alieleza mwananchi mwingine
mbele ya mbunge Kamonga
Kwa
upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Baraka
Mfaume aliyeongozana na mbunge katika mkutano huo amesema Chama
kimepokea changamoto hiyo na kuelekeza ofisi ya mkuu wa wilaya kuifanyia
kazi.
"Kwa desturi zetu
tunawaheshimu sana ndugu zetu waliotangulia mbele za haki,uongozi wetu
wa afya wamekuwa wakitutaarifu ndugu zetu wamefariki kwa tatizo gani ili
taratibu za mazishi zifanyike kwa tahadhari lakini kama jambo hili
halipo hivyo hapa tunaliacha kwa mkuu wa wilaya Lifanyiwe
ufuatiliaji"alisema Baraka Mfaume
Naye
mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga amesikitishwa na kitendo cha
wananchi hao kukabiliwa na changamoto hiyo huku akitaka viongozi wa
kijiji pamoja na afisa tarafa kuifuatilia changamoto hiyo na kutoa wito
kwa viongozi kutoa elimu kwa wananchi ili kutoana ni kero kwao
wanapopatwa na matatizo ya misiba.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...