Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amezindua rasmi Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) huku akiwataka Mwenyekiti na Wajumbe wanaounda Bodi hiyo kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kupata kitu kimoja kwa manufaa ya Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkoani Dar es Salaam, Prof. Kitila ameitaka Bodi hiyo kufanya vitu vyake kwa weledi sambamba na kuhakikisha inashauri ipasavyo Menejimenti ya ya Chuo hicho, kutunza nidhamu ya Menejimenti na kutatua changamoto za Chuo kwa ujumla.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud S. Kigahe ameitaka Bodi hiyo kuwa na uthubutu katika masuala yake ili kuleta manufaa kwa nchi na kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.

Pia amewaasa kufanya kazi kwa kushirikiana zaidi na kwa waledi pamoja na kukaa na Sekta Binafsi kupata mwafaka katika changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la ajira.
Prof. Kitila amezindua Bodi hiyo baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania June 8 mwaka huu, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Eleuther Alphone Mwangeni ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kuku cha Ardhi (ARU) sambamba na Wajumbe Sita watakaodumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
 
Rais kateua Mwenyekiti wa bodi ila Wajumbe wameteuliwa na Waziri wa Viwanda.
Wajumbe walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

1. Dkt. Consolatha Deogratias Ishebabi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo, Wizara ya Viwanda na Biashara;

2. Dkt. Kenneth Hosea ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;

3. Bi. Mwema Punzi ambaye ni Wakili wa Serikali Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

4. Bw. Zahoro Muhaji ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF);

5. CPA. Peter Lucas Mwambuja ambaye ni Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA);

6. Waziri amemteua Prof. Wineaster Saria Anderson ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mjumbe wa Bodi ya CBE.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...