RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameutaka Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha inavipatia maji safi na salama Vitongoji sita vilivyomo katika Shehiya za Muungoni na Kitogani sio zaidi ya Julai 30, 2021.

Dk. Mwinyi ametoa agizo hilo leo wakati alipokitembelea kituo cha maji kilichopo Kitogani, ambapo pamoja na mambo mengine alitaka kufahamu changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo, ikiwa  mwanzo wa ziara yake ya kuutembelea Mkoa wa Kusini Unguja.

Amewataka watendaji wa Mamlaka hiyo  kukamilisha mchakato wa kuvipatia huduma hiyo mapema iwezekanavyo kwa kukiwekea kituo hicho mundombinu kutoka Mradi wa Ras el Hemma wenye uwezo  wa kuzalisha lita Milioni moja ya maji kwa siku, sambamba na kukiwekea kituo hicho Paipu mpya ili kiweze kutoa huduma kwa ukamilifu.

Aliwataka Viongozi wa ZAWA kuwajibika na kuwawajibisha watendaji wote wanaoshindwa kutekeleza majukumju yao ipasavyo, akibainisha kuwepo utendaji dhaifu wa watendaji  katika mamlaka hiyo kwa kipindi kirefu.

Aliuagiza uongozi wa ZAWA kuhakikisha maeneo yote yanayomilikiwa na mamlaka hiyo, ikiwemo vituo vya maji yanapimwa na kupatiwa hati za umiliki.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema serikali itayafanyia matenegenzo majengo yote ya Skuli, ili kuona kunakuwepo mazingira bora ya upatikanaji wa elimu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...