Charles James, Michuzi TV
SIKU moja baada ya Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO) kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wake, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imetoa maagizo manne kwa baraza hilo.
Maagizo hayo ni matumizi bora ya sheria, uadilifu, weledi katika ufanyaji kazi zao huku ikisisitiza uajibikaji na uwazi katika utendaji kazi wao.
Serikali pia kupitia Wizara hiyo imewataka kulinda maslahi ya Nchi,kuwa sauti kwa Mashirika yote yasiyokuwa ya Kiserikali na pindi wanapotekeleza majukumu yao kuweka
mipaka ya kujisimamia.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Patrick Golwike alipokua akizungumza na uongozi wa baraza hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima.
Golwike Kaimu amesema Serikali kupitia Wizara inaipongeza kamati iliyosimamia uchaguzi huo kwa kufanya kazi kubwa ambapo amewataka viongozi wapya kusimamia sheria na kufuata misingi yote ya uanzishwaji wa Mashirika hayo huku akisisitiza uzalendo na kuweka maslahi ya Nchi mbele.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kamati teule ambayo ilisimamia uchaguzi,Flaviana Charles amesema mara baada ya kuchaguliwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Doroth Gwajima June 7 mwaka huu walihakikisha uchaguzi unafanyika katika Mikoa 26 na Wilaya 139 kwa kushirikiana na Ofisi za Msajili.
Nae Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Lilian Badi ameahidi kutekeleza majukumu yake kisheria kwa kufuata kanuni na muongozo huku akitekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa uchaguzi.
" Sisi kama uongozi wa baraza hili tunaahidi kuyatenda yale yote kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa lakini pia tukitimiza ahadi zetu tulizowaahidi wajumbe," Amesema Badi.
Jana Wajumbe wa Baraza hilo waliwachagua viongozi wapya wa NaCONGO ambao ni Mwenyekiti,Katibu Mkuu,Mwekahazina na Kamati za Maadili,Fedha na Utawala,Maendeleo na Uwezo,Utandaa na Mawasiliano na wajumbe wane wa Bodi.
Aliyekua Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya NaCoNGO, Flaviana Charles akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza jipya la mashirika yasiyo ya kiserikali baada ya kufanikiwa kuchafua viongozi wapya.
Mwenyekiti mpya wa NaCoNGO, Lilian Badi akitoa neno mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Patrick Golwike baada ya kuzinduliwa Kwa baraza hilo leo jijini Dodoma.
Wajumbe mbalimbali wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali NaCoNGO wakifuatilia uzinduzi wa baraza hilo baada ya Jana kufanya uchaguzi wake na kuwapata viongozi wapya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...