Charles James, Michuzi TV

IKIWA ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamia jijini Dodoma, Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) umezindua jengo lao katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Uzinduzi wa jengo hilo umefanywa leo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Dk Faustine Ndugulile ambapo ameupongeza mfuko huo kwa hatua zake za kuanza ujenzi wa jengo lao wenyewe.

Ujenzi wa jengo hilo la makao makuu ya UCSAF utagharimu kiasi cha Sh Bilioni 2 hadi kukamilika kwake ambapo Waziri Dk Ndugulile ameeleza kuridhishwa na kiwango hicho cha fedha kilichotengwa.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi kuashiria ujenzi huo, Dk Ndugulile ameeleza kufurahishwa kwa hatua hiyo huku akisisitiza kuwa ifikapo Desemba mwaka huu ataleta mgeni rasmi wa kuzindua jengo hilo ili lianze kutumika.

" Nimefurahishwa na hatua ya mfuko wetu huu kuamua kuwa na jengo lake wenyewe, hatua hii itapunguza kiasi cha fedha ambacho kilikua kikitumika katika jengo ambalo tulikua tunatumia ambalo halikua mali ya UCSAF.

Gharama zinazotumika hapa nimeridhishwa nazo na ninaamini thamani ya fedha 'value for money's itaonekana, nisisitize tu kwamba ifikapo Desemba mwaka huu tuhamie hapa na nitaleta mgeni rasmi wa kuja kutuzindulia hata kama tutakua hatujamaliza tuhamie hivyo hivyo," Amesisitiza Waziri Ndugulile.

Amesema ni jambo la kupongezwa kuona taasisi kama UCSAF ikiunga mkono azma ya Serikali ya kuhamishia makao makuu yake Dodoma na kuona kwamba hata wao wanapaswa kuwa na jengo lao la makao makuu yao kama zilivyo taasisi zingine za Umma.

Dk Ndugulile amesema watu wote wanatambua kwamba mawasilino kwa sasa sio anasa ni haki ya kimsingi ya kila mtanzania na kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote lengo kuu ni kuhakikisha kwamba wanapeleka mawasilino katika maeneo yote na kona zote za nchi

Hata hivyo amesema Mfuko wa Mawasilino kwa wote ulianzishwa kwa mujibu wa sheria mwaka 2007 lakini walianza majumu na operation  zake mwaka 2009

Amesema Majukumu yake ni kuhakikisha wanapeleka mawasiliano maeneo  ambayo hayana mvuto wa kibiashara na maeneo ya pembezoni mwa nchi ambapo amedai kuna  Makampuni ya simu ambayo   yanaangalia maeneo  kwa ajili ya uwekezaji ili yaweze kupata faida.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba amesema mradi huo wa ujenzi wa makao makuu ya Mfuko huo ulianza Februari 15 mwaka huu na kwamba wanategemea ndani ya kipindi cha miezi Saba wawe wamemaliza na kuhamia.

 " Mhe Waziri tunategemea kutekeleza mradi wa ujenzi wetu ndani ya muda tulioupanga ambapo hadi kufikia Novemba mwaka huu tutakua tumemaliza ujenzi na Desemba watumishi waweze kuhamia ili tuanze kazi tukiwa kwenye jengo letu wenyewe.

Ujenzi huu ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi na azma ya Serikali kuhamia Dodoma hatua ambayo ilianzishwa na aliyekua Rais wetu Hayati Dk John Magufuli na sasa inaendelezwa vema na Rais Samia Suluhu Hassan na sisi tunaahidi kuendelea kutekeleza azma hiyo," Amesema Mashiba.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameupongeza mfuko huo kwa hatua hiyo huku akiwaahidi ushirikiano pamoja na ukamilifu wa miundombinu ya kuweza kufikika zilipo ofisi hizo.

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia, Dk Faustine Ndugulile akiongoza zoezi la uwekaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la makao makuu ya UCSAF eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo.

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia, Dk Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa tukio la uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa jengo la makao makuu ya Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote UCSAF leo jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote UCSAF, Justina Mashiba akizungumzia ujenzi wa jengo la makao makuu ya Mfuko huo baada ya Waziri Ndugulile kuweka jiwe la msingi leo.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia, Dk Faustine Ndugulile wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza shughuli ya uwekaji jiwe la msingi kwenye jengo la makao makuu ya UCSAF jijini Dodoma leo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...