Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amewahakikisha wananchi ambao maeneo yao yatapitiwa na mradi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Fela Mwanza hadi Isaka Shinyanga kuwa watalipwa fidia kwa mjibu wa Sheria.
Aidha ameongeza kuwa mradi huo utatoa fursa nyingi za kiuchumi kwa wananchi ikiwemo ajira zaidi ya elfu kumi pamoja na zabuni za utoaji huduma na usambazaji bidhaa mbalimbali kama vyakula pamoja na usafiri/ usafirishaji.
Mhandisi Gabriel ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya kuwajengea uelewa wananchi kuhusu utekelezaji wa mradi wa SGR kutoka Fela hadi Isaka ambayo imeanza Julai 06, 2021 ambapo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuwasikiliza wataalamu kutoka Shirika la Reli nchini (TRC) watakapopita katika maeneo yao.
Juni 14, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo ambao hadi kukamilika utagharimu takribani shilingi trioni tatu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...