KATIKA jitihada za kuimarisha afya na kuongeza ufanisi zaidi wa utendaji kazi kwa watumishi wake, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (PO-TSC), imejiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku ya Ijumaa kuanzia saa kumi na nusu jioni.

 

Akiongoza mazoezi hayo kwa watumishi, Katibu wa PO-TSC, Paulina Nkwama alieleza kuwa ofisi yake imekuwa ikiunga mkono agizo la Serikali la kufanya mazoezi ikiwa ni moja ya njia za kujikinga na magonjwa mbalimbali yasiyo ya kuambukiza na kuimarisha afya.

 

Aliongeza kuwa pamoja na kuimarisha afya, watumishi hao wanapokutana na kufanya mazoezi kwa pamoja inawasaidia kujenga upendo na ushirikiano miongoni mwao na hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. 

 

"Naendelea kuwasisitiza tujitokeze kwa wingi kwenye mazoezi na michezo kwani michezo na mazoezi ni afya, ni urafiki, ni ajira kwa wasio na ajira, na pia ni mshikamano." Alisema Nkwama.

 

Mazoezi hayo yanayofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...