Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa
(Mb) amemuomba Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Mhe. Mhandisi
Aisha S. Amour kuendeleza Uhusiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya
Tanzania na Kuwait, kwa kuona jinsi gani pia Taifa hilo linaweza
kusaidia kuboresha miundombinu katika Shule mbalimbali za Michezo
nchini.
Mhe.Bashungwa ameyasema hayo leo tarehe 13 Julai, 2021
alipokutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Aisha katika moja ya kumbi za
uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo pia amemuhakikishia Mheshimiwa Balozi
kuwa Wizara ipo tayari kushirikiana naye bega kwa bega katika masuala
yote ya kimichezo yatakayoendeleza ushirikiano mwema baina ya nchi hizo
mbili.
“Mheshimiwa Balozi kwanza tu nikuhakikishie kuwa Wizara
ipo tayari kushirikiana nawe katika masuala yote ya kimichezo ambayo
yataendeleza ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Kuwait, lakini pia
tuomba utusaidie kuona ni kwa jinsi gani Taifa hilo litatusaidia
kuboresha miundombinu katika shule zetu za michezo nchini, ili kuendelea
kuibua vipaji zaidi mashuleni na hususani katika mashindano ya Umisseta
na Umitashumta,”amesema Mhe. Bashungwa.
Kwa upande wake Mhe.
Aisha Amour amesema Serikali ya Kuwait ipo tayari kuendeleza Uhusiano
mzuri uliopo kwa kushirikiana na Tanzania katika michezo pamoja na
Sanaa, huku akisisitiza kufanyika kwa mchezo wa Kirafiki wa mpira wa
miguu baina ya timu za mataifa hayo, jambo ambalo litatangaza Utalii na
kupelekea ajira ya wachezaji nje ya nchi.
“Mheshimiwa waziri
nikuombe ulisimamie hili la kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya mataifa
haya mawili, kwa sababu wenzetu wapo tayari, na hii itatusaidia pia
kukuza uchumi wetu kwa kuingiza fedha za kigeni pamoja na kutangaza
Utalii tulionao nchini, na labda pia wachezaji wetu wanaweza kupata soko
nje ya nchi kwa kupitia ushirikiano huu,”amesema Mhe. Aisha.
Home
BIASHARA
WAZIRI BASHUNGWA AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KUWAIT KUBAINISHA JINSI GANI WATASHIRIKIANA KUKUZA SEKTA ZA MICHEZO NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...