Namwandishi wetu

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umepongezwa kwa kuibuka mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Bima na Hifadhi ya Jamii zilizoshiriki kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya hafla ya ufungaji wa maonesho hayo, mmoja wa wadau ameeleza kuwa ushindi huo ni chachu kwa Mfuko kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wadau wake ikiwemo kujitangaza kupitia maonesho na makongamano yanayohusisha wadau tofauti nchini.

“Nawapongeza sana WCF kwa kuibuka washindi wa pili, binafsi niliposikia wapo sabasaba nilisema ni lazima niwatembelee, na kwa kweli wamenihudumia vizuri sana. Ninashauri wasiishie kushiriki sabasaba tu, waendelee kujitangaza kupitia makongamano ya wadau, alisema Athuman Saidi, mmoja ya waliotembelea banda la WCF.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF  Dkt. John Mduma, baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo amesema ushindi huo umezidi kuwapa motisha zaidi kuendelea kutoa huduma za fidia stahiki na kwa wakati pamoja na elimu ya taratibu za madai ili kuepukana na vikwazo vinavyochangia Mfanyakazi kukosa sifa ya kulipwa fidia yake.

Pia ameahidi kufanyia kazi maoni yaliyowasilishwa na wadau waliotembelea banda la Mfuko huo kwa lengo la kuendelea kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika katika utoaji wa huduma za fidia.

"Katika maonesho haya tumekuwa washindi  wa pili kwetu ni wajibu mkubwa tumepewa katika kuonesha tofauti kati ya mshindi na asiyeshinda lakini zaidi ushindi huu unapaswa kuwa na tija katika utoaji wa huduma za fidia ili kuendelea kuwa mfano wa kuigwa," amefafanua.

Tuzo hiyo ilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa sherehe za kufunga maonesho hayo zilizoenda sanjari na utoaji wa zawadi kwa washindi wa makundi mbalimbali.

Katika Maonesho ya 45 kundi la Bima na Taasisi za Hifadhi ya jamii lilijumuisha  taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambapo maboresho makubwa yaliyochangia WCF kupata ushindi  kwa mwaka huu ilikuwa ni pamoja na kutekeleza mapendekezo ya wadau wa sekta binafsi ya punguzo la viwango vya uchangiaji pamoja na kuimarisha matumizi ya huduma za kimtandao katika utoaji wa huduma za  Fidia.

Maonesho haya yaliyobeba kauli mbiu isemayo "Uchumi wa Viwanda, Ajira na Biashara Endelevu"yalifunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango mnamo Julai 5, 2021 ambapo nchi mbalimbali zilishiriki maonesho ya mwaka huu ikiwemo China, Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE), Marekani na Uturuki.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (Katikati) akiwasikiliza wananchi waliotembelea kwenye band a la Mfuko huo ili kupata elimu ya fidia wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofikia kilele jana. Mfuko huo umeibuka mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Bima na Hifadhi ya Jamii.

Mdau wa WCF akipatiwa huduma kwenye banda la Mfuko.
Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge (katikati) akitoa elimu kwa wananachi waliotembelkea band ala Mfuko Julai 13, 2021


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...