Na Mwandishi wetu 

KATIBU Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema utulivu na uimara wa Chama chao ni matokeo ya kuimarika kwa demokrasia ya ndani ya Chama hicho, hivyo viongozi na wanachama wamesisitizwa kuheshimu na kufuata taratibu ambazo wamejiwekea hasa wakati kikielekea chaguzi za ndani.

Chongolo amesema hayo alipokuwa akihutibia viongozi na watendaji mbalimbali wa Chama na serikali katika kikao cha majumuisho ya ziara yake  mkoani Mbeya amesema miongoni mwa sababu nyingine inayoongeza imani ndani ya  CCM na kukubalika kwake ni  kutokuwepo kwa makundi pamoja na uadilifu na uwajibikaji kupewa msukumo wa kipekee ndani na nje ya CCM. 

Amesema   katika kuendelea kuhimiza umoja na mshikamano ndani ya chama hicho ni lazima  wanachama wapewe nafasi ya kusikilizwa badala ya kuonekana   wanapotoa maoni  yasiyowapendeza viongozi kuonekana  wasaliti na kutengenezewa mizengwe.

Chongolo amesema Chama lazima  kiwe kinafanya vikao na kuhakikisha vinakuwa vyenye agenda za maendeleo na sio kujadili watu, majungu au kuendeleza siasa za makundi.

Aidha wakati  Chama hicho kikielekea katika uchaguzi wa ndani si vyema  wanachama kutengenezewa tuhuma za kupika ili wakose sifa za kuomba uongozi ndani ya chama jambo ambalo sio sawa na chama kitakuwa makini kuhakikisha wanachama hawaonewi na haki inatendeka.

Amesisitiza CCM imeendelea kubaki kuwa tumaini pekee la watanzania ikiwa ni matokeo ya chama chao  kujisahihisha na kurejesha imani kubwa kwa wananchi kwa kuisimamia serikali kwa ufanisi mkubwa katika kuboresha huduma za kijamii, upatikanaji wa haki, kudhibiti vitendo vya wizi, rushwa, ufisadi.

Pia kukemea vikali matumizi mabaya ya madaraka, ulinzi wa rasilimali za nchi, kuukabili utendaji kazi wa mazoea na matumizi yenye tija kwa mapato ya serikali" alisema chongolo.Chongolo na Sekretarieti yake ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamehitimisha ziara yao katika mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...