Aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya kahama kwa mwaka 2017/19, Samson Lutema Lutonja amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na chama cha mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa jimbo la ushetu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo muda mfupi baada ya kuchukua fomu katika ofisi za chama cha mapinduzi wilayani hapa Lutonja amesema amedhamiria kuwaunganisha wananchi wa jimbo ushetu katika sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
“Nitaanzia pale alipoishia mtangulizi wetu aliyetangulia mbele za haki kama chama changu kikiniparidhaa ya kugombea jimbo la ushetu,Elias Kwandikwa alifanya mambo mengi katika jimbo hili,nitayaishi mazuri yake,”alisema Lutonja.
Amesema kuwa kupitia uzoefu alioupata ndani ya chama wakati akiongoza umoja wa vijana wilaya ya kahama (UVCCM) utamsaidia kuongoza kwa weledi pindi atakapopata nafasi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...