Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Chama  cha Mapinduzi CCM,Daniel Chongolo amesema kuwa Chama hicho ni kikubwa kuliko mtu yoyote,hivyo hakuna pembe zaidi na hao wanaaofikiria  kushindana wameshaanza  kuchukuliwa hatua.

Kauli ya Chongolo inakuja kukiwa na wimbi la kauli kizani zinazotolewa na baadhi ya wanachama wa Chama Chama wakiwemo baadhi ya Wabunge ambao wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali zinazokwenda tofauti na msimamo wa Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na Janga la Uviko 19 ikiwemo uchomaji wa Chanjo.

Amesema kwamba katika Chama hicho ukiondoka Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti anayefata kwa ukubwa  ni nafasi ya Katibu Mkuu lakini bado na yeye hana  mamlaka ya kuweka mambo yake kwani Chama kinauwezo wa kumchukulia hatua.

" Hiki ni Chama kikubwa kuliko mtu yeyote hata mimi sina Mamlaka ya kuweka  mambo yangu sasa sijui baada  kwenye Chama hiki baada ya  Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti sidhani kama kuna mtu mwenye pembe zaidi,"amesema na kuongeza

"Chama hiki kina utaratibu wake wa kumuwajibisha mtu yeyote,hata mimi Mtendaji mkuu nikifanya mambo ya hovyo nitawajibishwa ,hivyo mtu yoyote asidhani anaweza kuota pembe kuliko wengine,"alisema


Kuhusu Katiba Mpya 


Chongolo amesema hakuna Mwananchi ambaye anayebeba bango la kudai Katiba Mpya zaidi ya wanasiasa ambao wanamasilahi yao binafsi.

Amesema masilahi hayo ambayo yamegawanyika katika sehemu tatu ikiwemo yakutaka  Tume Huru ya Uchaguzi, demokrasia na uhuru."Tuambie sisi kwani  hatuna uhuru?,"amehoji

Aidha amesema Chama hicho nimetoa maelekezo kwa serikali kupitia Halmashauri mbalimbali pamoja na manispaa kuhakikisha zinajenga madarasa na kuboresha miundombinu ya elimu kli wanafunzi waanze masomo kwa wakati.

Amesema kumekuwa na utaratibu wa kucheleweshwa ujenzi wa madarasa na hivyo wanafunzi kushindwa kuanza masomo kwa wakati jambo ambalo kwa sasa Chama hicho hanitaki kuona hali hiyo ilitokea.

"Utoaji elimu bila malipo liwe na tija zaidi ni lazima kuwe na miundombinu rafiki kwa wanafunzi, kwamba wanafunzi wanapoandikishwa waikute miundombinu yote ya kujifunzia inakuwa tayari" amesema na kuongeza

"Suala la miundombinu ya kujifunzia ikiwemo madarasa, madawati,fedha zake zitatolewa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha, lengo ni kuondoa usumbufu wa kukimbizana na watendaji hata kufikia hatua ya kuzuia likizo zao. Changamoto hii tunataka kuimaliza mapema"Daniel Chongolo


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...