Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga  Halima Bulembo amewasilisha taarifa  ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka  2020 - 2025 kwa kipindi  cha Januari hadi juni 2021.

Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM wilayani Muheza ,Bulembo Alisema  mojawapo ya mafanikio  ni utoaji wa mikopo  kwa vijana,wanawake  na watu wenye ulemavu isiyo na riba kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Jumla ya vikundi 55 vimepata mikopo  yenye thamani ya shilingi million 337,000,000.

 Vikundi vya vijana  vimepata sh .152,000,000/= wanawake sh .152,000,000 na watu wenye ulemavu  33 wamenufaika.

Pamoja  na mikopo hiyo mafunzo ya stadi za ujadsiriamali yametolewa na vijana 276,wanawake 324 na watu wenye ulemavu  33 kutoka katika 20 na shughuli za kiuchumi167za vijana,wanawake na makundi emengine zimerasimishwa.

Aidha wajasiriamali 473  wamewezeshwa kukuza uzalishaji na mitaji.

Mikopo hii imeweza kuzalisha fursa za ajira 473 kwa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...