Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha bei ya zao la Alizeti kupanda hadi Sh 1600 kwa Kilo Moja lakini akaihoji Serikali imejipangaje kuwawezesha wakulima wa zao hilo kupata mbegu bora na za kisasa.

Ditopile ameuliza swali hilo leo Bungeni wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu ambapo Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema tayari Serikali ishaingia mkataba na wasambazaji wa mbegu kwa ajili ya kusambaza mbegu bora za zao hilo.

" Niipongeze sana Serikali yetu kwa muda mfupi tu imeweza kupandisha thamani ya Zao la Alizeti ambapo bei imepanda hadi Sh 1600 kwa Kilo Moja, hii haijawahi kutokea kwenye Nchi yetu, kupanda huku kwa bei kumesababisha muamko uwe mkubwa kwa watu kwenda kulima Alizeti, Je Serikali imejipangaje kuhakikisha inawezesha upatikanaji wa mbegu bora kwa ajili ya msimu mpya wa Kilimo hasa kwa wakulima wetu wa Dodoma,"?

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kwa sasa Serikali imeanza kuchukua mahitaji ya Mikoa wanayoleta wenyewe kutokana na uwezo wa Mkoa husika katika suala la uzalishaji ambapo katika Mkoa wa Dodoma wanashirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia Katibu Tawala wa Mkoa.

" Kwa sasa tunashirikiana na Ofisi ya RAS kutuletea mahitaji ya Wilaya zote ili sisi kama Wizara tuweze kuwapatia mbegu, nataka niwahakikishie wakulima tutahakikisha wakulima wa Alizeti wanapata mbegu bora ambazo zitaweza kuwasaidia mwaka huu wakati ambao sisi Serikali tunajipanga kwa mwaka mwingine," Amesema Bashe.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile akizungumza katika kikao cha Bunge kilichoanza leo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...