Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhe. Zahara Michuzi ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo unaojengwa eneo la Magogo mjini Geita (pichani chini) na kueleza kuwa mpaka kufikia mwezi wa 11 ujenzi huo kwa awamu ya kwanza utakuwa umekamilika kwa asilimia 98% mpaka 100%.
Mhe Zahara amesema hilo linawezekana kwa sababu fedha ipo, mkandarasi yupo na vifaa vipo na vinafika saiti kwa wakati na kufikia tarehe 1 mpaka 15 ya mwez wa 11 uwanja huo utakuwa umekamilika kwa ajili ya matumizi.
"Matamanio yangu katika ujenzi wa uwanja (Geita Gold Stadium) ni kwamba mechi zote za Ligi Kuu na michuano mingine zinachezewa hapa ili wananchi wa Geita waweze kupata burudani na shangwe hili la Ligi Kuu wakiwa nyumbani wakiangalia live"
"Sambamba na hilo naamini kupitia shangwe hilo la Ligi Kuu tutapata wageni wengi sana ambao watatumia huduma mbali mbali ikiwemo hotel zetu watoa huduma za chakula pamoja na wenye vyombo vya usafiri, tunatamani kuona mzunguko wa fedha unakuwa mkubwa na shughuli za kimaendeleo zinakuwa zaidi."
"Kwa kweli niwahakikishie wana geita wenzangu kwamba mkandarasi huyu wa sasa hivi kwanza anavifaa vya kutosha na pia kutokana na ukaguzi wetu wa mara kwa mara na wahandisi wetu muda mwingi tuko saiti kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kutokana na mipango mikakati ya kazi zao." ameeleza Mhe. Zahara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...