SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imendelea kuwekeza kwenye Taasisi zinazohusika na utafiti na uzalishaji wa mbegu bora ikiwa ni pamoja na mbegu za zao la Alizeti ili kuongeza tija na kukabiliana na upungufu wa mafuta kula nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (MB) tarehe 15 Agosti, 2021 kwenye hafla ya kufunga rasmi Kongamano la Wadau wa Alizeti Mkoani Singida liloambatana na Maonesho madogo ikiwa ni utekelezaji wa mradi ambao unafadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) kupitia Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC.)

Mhe. Kigahe amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imeamua kutoa kipaumbele kwa kuweka jitihada ya kuinua sekta ya mafuta ya kula nchini hususan sekta ndogo ya zao la Alizeti kwa kuwekeza kwenye tafiti za mbegu zenye ubora na uwezo wa kuzalisha mafuta kwa wingi.

Ameongeza kuwa Serikali imeongeza bajeti ya Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutoka Shilingi bilioni 7.35 mwaka 2020/2021 hadi shilingi  bilioni 11.63 mwaka 2021/20222.

“ bajeti ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) imeongezeka kutoka bilioni 5.42 mwaka 2020/2021  hadi shilingi bilioni 10.58 mwaka 2021/2022 kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mbegu bora zikiwemo mbegu za mazao ya mafuta  ya kula ” Alisema Mhe. Kigahe.

Mhe. Kigae amewataka Wakulima na Wasindikaji wa za zao la Alizeti kuchangamkia fursa hiyo kwa kuungana na kufanya kilimo cha mkataba ili Wakulima wapate uhakika wa soko la zao hilo na Wasindikaje wawe na uhakika wa upatikanaji wa malighafi.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah amesema kwenye Kongamano hilo imefanyika mikutano ya ana kwa ana yani (B2B) ambapo, Wakulima na Wasindikaji wameweza kukutana, kutambuana na kufanya makubaliano ya kuuziana punje za Alizeti hivyo kuondoa Madalali ambao wamekuwa ni kero kwa Wakulima na Wasindikaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...