MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Mchekeshaji Idrisa Sultan(27) na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kurusha maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Sultani ameachiwa huru na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Rubologa baada ya wakili wa Serikali Neema Mushi kudai kuwa DPP amewasilisha Nolle chini ya kifungu cha 91(1) cha CPA kuonesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Hakimu Rubologa alisema kwa kuwa DPP ameona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo, mahakama yake inakubali ombi la Jamhuri inawaachia huru washtakiwa.
 
Mbali na Idrisa, washtakiwa wengine ni Doctor Ulimwengu(28) na Isihaka Mwinyimvua(22).

Katika kesi hiyo inadaiwa kati ya Machi 8,  2016 na Machi 12, 2020 sehemu tofauti tofauti  jijini  Dar es Salaam washitakiwa hao, walirusha maudhui online tv  kwenye akaunti ijulikanayo Loko Motion bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini( TCRA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...