Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameitaka Jamii kuachana na imani potofu kuwa pembe za faru zinaongeza nguvu za kiume kwani hakuna uthibitisho wa kisayansi juu ya madai hayo baadala yake ameitaka Jamii kuungana na Serikali katika kumlinda faru ambaye ni kivutio kikubwa cha utalii hapa nchini.

Amesema kutokana na imani hiyo potofu imepelekea faru kuwindwa sana na kuna baadhi ya nchi zimekuwa zikinunua pembe hizo za faru kwa bei ya ajabu, hali hii imeilazimu Serikali ya Tanzania kujizatiti katika kuwalinda faru kwa kuwawekea vifaa maalum ajili ya ulinzi ili wasiweze kuuawa

Ametoa kauli hiyo wakati akizindua zoezi la uwekaji wa alama pamoja na vifaa maalum kwa faru katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa Wanyama hao ambao ni zao kubwa la Utalii nchini

Dkt.Ndumbaro amesema kuhifadhi faru kunataka nguvu ya ziada pamoja na akili ya ziada kwa sababu binadamu ni kiumbe mharibifu na tayari ameingiza mawazo yake kuwa nyara zina nguvu ya ziada.

Kufuatia hali hiyo ameaugiza Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ushirikiane na Idara ya Wanyamapori kuhakikisha wanakamilisha kuweka alama na vifaa maalum kwa ajili ya utambuzi na ulinzi kwa faru wapatao 45 badala ya kuwawekea vifaa hivyo faru 20 pekee waliokuwa wamepanga kuanza nao lengo likiwa ni kuhakikisha faru wote katika eneo hilo wanakuwa salama zaidi

Dkt.Ndumbaro ameeleza kuwa faru wote wanatakiwa kuwekewa vifaa hivyo kwa sababu wale 25 kati ya 45 ambao watakuwa wamesalia wanaweza kukutana na balaa yoyote

Ambapo ameutaka Uongozi wa Hifadhi ya Ngorongoro kama una changamoto yyoyote wamfikishie ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa faru wote kwa sababu mitambo iliyopo ina uwezo wa kufuatilia nyendo za faru zaidi ya 100,000 kwa ajili ya usalama wao.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameuagiza Uongozi wa Hifadhi ya Ngorongoro kuhakikisha faru wenye watoto wadogo wanahifadhiwa katika maeneo maalum hadi pale faru wadogo watakapokuwa wakubwa ndipo waweze kurudishwa katika mazingira yao asili ili wasiweze kuliwa na fisi

Kwa mujibu wa taarifa fisi wamekuwa tishio kubwa kwa watoto wa faru ambapo faru wanapokuwa wadogo wamekuwa wakiliwa na fisi ambapo katika eneo la Ngorongoro kuna idadi kubwa sana ya fisi

Amefafanua sababu za kuliwa na faru wadogo ambapo amesema faru wenye watoto wadogo huliwa kwa sababu faru weusi kiasili huacha watoto wadogo nyuma wakati wa kutafuta malisho hivyo fisi hutumia nafasi hiyo kuvamia na kuwala watoto hao.

Amesema kutokana na umuhimu wa fisi kiikilojia na kiutalii haiwezekani kuwaondoa fisi ila jambo linalotakiwa kufanywa ni kuhakikisha faru watoto wanalindwa kwa kuwaondoa katika mazingira hayo hatarishi.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameagiza Uongozi wa Hifadhi hiyo kutenga eneo maalum kwa ajili faru wazee ambao kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu kuwa faru wanapozeeka hupoteza uwezo wa kuona hivyo litengwe maalum kwa ajili ya kuwahufadhi faru hao ili litumike kwa ajili ya utalii wa faru.

Awali, Kamishna Uhifahi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro , Dkt.Freddy Manongi amesema Ngorongoro ni eneo pekee dunia ambalo watalii wataweza kumuona faru weusi katika mazingira yake asilia

Aidha, Dkt.Manongi amueleza changamoto wanazokabiliana katika kumlinda faru kutoka na ûwepo matumizi mseto katika eneo hali inayochangia katika kuwalinda faru hao.

Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Maurus Msuha ameeleza kuwa zoezi la kuweka alama kwa Faru ni utekelezaji wa mpango wa kimataifa wa kuhakikisha kuwa maeneo yote yanayopatikana faru yanalindwa kwa mbinu za kisasa na faru hao kuwekewa alama za utambuzi ili kuwafuatilia mienendo yao kwa urahisi zaidi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( katika ) akiwa kwenye picha ya  pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Wadau wa Uhifadhi nchini  mara baada ya kushuhudia  zoezi la  uzinduzi wa uwekaji wa alama pamoja na vifaa maalum kwa ajili ya utambuzi na kufuatilia nyendo za faru kwa ajili ya ulinzi wa faru hao katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...