Na Mwandishi wetu, Hanang’


HANANG' Vijana Jogging Club imezinduliwa rasmi na Mbunge wa Vijana Taifa kupitia Mkoa wa Manyara, Asia Halamga na kuhusisha wananchi mbalimbali wa eneo hilo.

Asia akizungumza baada ya kuzindua mazoezi hayo amesema kufanya mazoezi ni jambo jema kwani wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza ufanywaji wa mazoezi.

Amewataka vijana wa eneo hilo kuendeleza mazoezi hayo kila mara kupitia uzinduzi huo kwani mazoezi yatawajengea kiafya na kuwaweka pamoja.

"Hata Serikali imeanzisha utaratibu wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa kuhakikisha watumishi wa Serikali na wananchi kwa ujumla wanafanya mazoezi hata walau mara moja kwa mwezi," amesema Asia 

Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Janeth Mayanja amewapongeza vijana hao kwa kujitolea kushiriki mazoezi hayo ili kuweka miili yao vizuri kwa ajili ya manufaa ya afya zao.

“Kama mnavyofahamu hivi sasa tunaendelea kuchukua tahadhari ya maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19 na wataalamu wa afya wanatuhimiza kufanya mazoezi,” amesema Mayanja.

Mbunge wa vyuo vikuu Dkt Pauline Nahato, amewapongeza washiriki wote kushiriki mazoezi hayo na ndiyo sababu naye akawaunga mkono kwani hilo ni jambo zuri.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang'  Paul Bura amwewataka washiriki wa jogging hiyo kushiriki mazoezi kila mara ili kupiga vita vitambi.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hanang’ Yohane Leonce alisema wanafanya utekelezaji wa agizo la Katibu mkuu wa UVCCM Taifa, Kenani Kihongosi alilolitoa la kila wilaya kuanzisha klabu za jogging.

Jogging hiyo imewashirikisha vijana wa eneo hilo, askari polisi, mgambo, baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari, msingi na wananchi kwa ujumla.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...