Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini pindi wanapoona jambo lisilo la kawaida ili kuweza kuchukuliwa hatua za haraka kabla ya kuleta madhara kwa jamii.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa gwaride maalum la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Jeshi hilo akiwemo Balozi Valentino Mlowola, Robert Boaz aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini, Dare s salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kumalizika kwa gwaride hilo pia IGP Sirro amezungumzia suala la mtu aliyewashambulia askari Polisi kwa risasi na kuwaua na baadae mtu huyo nae kuuawa amesema Jeshi hilo limemaliza taratibu zake hivyo familia inaruhusiwa kuuchukua mwili wa kijana huyo kwa ajili ya taratibu nyingine.

Kwa upande wake Kamishna Mstaafu Robert Boaz amesema licha ya kustaafu utumishi wa umma lakini bado ataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea kutenda kazi zake kwa weledi na kwa kufuata misingi ya kanuni na taratibu zilizopo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...