Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Said Mndeme akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na namna ya kupata makazi katika nyumba za Magomeni Kota na kujiepusha na matapeli wanaojifanya kuwa ni maafisa au wafanyakazi wa wakala hiyo wanaowataka wananchi kutoa fedha kinyume na taratibu za wakala hiyo, leo mkoani Dar s Salaam.

Muonekano wa nyumba za makazi Magomeni Kota mkoani Dar es Salaam.


WAKALA Wa Majengo Tanzana (TBA,) imewataka wananchi kujiepusha na matapeli wanaojifanya maofisa na wafanyakazi wa wakala hiyo na kuwataka  watoe fedha ili waweze kupangishwa au kuuziwa nyumba za makazi za 'Magomeni Kota' ambazo hadi sasa kwa kiasi kikubwa zimekamilika, huku utekelezaji wa uliobaki ukiwa ni umeme na lifti pekee.


Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Said Mndeme amesema, kumekuwa na utapeli unaofanywa na baadhi ya watu kupitia mradi huo ambapo wamenasa sauti na baadhi ya taarifa za baadhi ya watu wanaojifanya maofisa na wafanyakazi wa wakala hiyo wakiwataka wananchi kutoa fedha ili waweze kupangishwa au kuuziwa nyumba hizo jambo ambalo si kweli na si utaratibu wa Wakala wa Majengo Tanzania.

" Utaratibu wa kupata nyumba hizi za makazi upo wazi na unatolewa katika ofisi zetu za TBA kitengo cha Miliki na si vinginevyo, wananchi wanaohitaji makazi katika nyumba hizo wanatakiwa kufika katika ofisi za TBA kupata maelekezo pamoja na fomu za maombi  huduma ambazo hutolewa bure bila malipo yoyote, na hadi sasa tumewahudumia watu 2000 wenye uhitaji wa vizimba vya biashara  bila malipo yoyote hivyo kupitia tamko hili tunawafumbua macho wananchi wasihadaike na kuingia mkenge na kwa wale waliotapeliwa wanaweza kufungua kesi ili kupata stahiki zao.......Tumenasa sauti na taarifa mbalimbali za utapeli huu ikiwemo ya mtu anayejiita Simon Gwamaka wakitumia Wakala wa Majengo Tanzania kutapeli watanzania tunasisitiza TBA haihusiki na udanganyifu huo.'' Amesema.

Pia amesema wamechukua hatua za kisheria kupitia kituo cha polisi Magomeni na wataendelea kutoa tahadhari kwa umma kupitia matangazo mbalimbali.

Aidha amesema kuwa, tangu mwaka 2017 mradi wa ujenzi huo unaosimamiwa na TBA uliasisiwa na Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Joseph Magufuli  na kuwalenga wakazi 644 ambao makazi yao yalibomolewa na kujengwa nyumba za kisasa ambazo zimekamilika kwa asilimia kubwa na utakabidhiwa  wakati wowote kuanzia sasa. 


Amesema, hadi sasa TBA imepokea maombi yapatayo 2000 ya wananchi wanaohitaji huduma za kupata maeneo ya bishara katika makazi hayo na utaratibu umewekwa wazi kwa nafasi zitakazobaki ambazo zitatolewa kwa utaratibu kutoka mamlaka husika.

Hayati Rais Dkt. John Joseph Magufuli aliwahaidi wakazi wa Magomeni Kota kukaa bure kwa miaka mitano bila kulipa kodi ya pango kwa miaka mitano huku gharama za uendeshaji ikiwemo umeme na maji zikiwa juu yao na wanatarajiwa kuhamia katika makazi hayo muda wowote kuanzia sasa kutokana na kukamilika kwa makazi hayo kwa kiasi kikubwa na yatakabidhiwa kwa Serikali muda wowote kuanzia sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...