Alisimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin
Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, Ndipo akajitolea
maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu na utu.
Siku hii huadhimishwa kila mwaka,
ili kuingiza thamani ya mafundisho hayo, ndani ya nafsi zetu. Imam Hussain
(a.s) alisimamia; Kuamrisha mema na kukataza mabaya. “Amr bil Marouf na Nahyanil
Munkar”
Utauliza kwanini
kuna matembezi haya leo katika ardhi ya Tanzania?
Ni Kwa sababu ya ujumbe wa amani aliyokuwa
amebeba Imam Hussain (as), Naye anaeleza, Mimi sikua sikwauovu au tabia mbaya wala
kutafuta umaarufu bali nilinyanyuka kutafuta kusawazisha mwenendo takatifu la
babu yangu, ambaye ni mjumbe wa Allah
(swt).
Imam Hussain(as), ni moja katika masahaba wa
Mtume (s.a.w.w), moja kati ya masharifu akatoka kuelekea katika ardhi ya
Karbala, akakubali aafe ili waislamu wawe kitu kimoja. Lakini si hivyo tu; umoja wa kiwanadamu, umoja
wa kiutu ulikuwa umesambaratika kipindi hicho na wakatih uwo.
Imam Hussain (as) katika msafara wake walikwepo waislamu wa madehebu zote na
pia watu wasioku wawaislamu.
Alikwepo mtumoja aitwaye John; ambaye sio mwislamu wala sio jina la
kiislamu. Kwa hivyo kutoka kwa Imam hussain (as) kulikuwa funzo ya kuleta umoja
kwa binadamu wote. Pasipo kuwa na kubagua dini zao, pasina kuangalia rangi zao;
ni mabadaliko kwa ajili ya waislamu, ni mabadaliko kwa ajili ya utu na mwandamu.
Waislamu, Wakristo, ma Yahudi, ma pagani, hawa wote waliungana na Imam Hussain
(as).
Leo hii dunia inahitaji amani. Amani imesambaratika, upendo umesambaratika.
Lengo la kutoka kwa matembezi haya kwa ajili
ya Imam Hussain (as) nikutaka kunyanua sauti kwamba amani, utlulivu na upendo ni
moja ya jambo muhimu na lienziwe na liangaliwe kwa makini.
Jumuiya ya Khoja Shia Ithanasheri ni nini?
Jumuiya hii ya waislamu, Khoja Shia Ithanasheri inatoa misaada nyingi ya
kibinadamu na msaada kwa watu wa Tanzania kwa ujumla. Wanaendesha hospitali ya Ebrahim
Haji iliyopo katikati mwa mji, ambacho kina bei ya chini sana na huduma bora.
Hivi majuzi pia tulifungua kituo cha macho ambapo wanabei za chini na hufanya
shughuli za jicho bure pamoja na kufanya opereshen wa mtoto la jicho (cataract),
tupo Temeke karibu na Chuo cha Bandari
na hudumia maeneo yaliyozunguka. Pamoja na hili, wanashirikana na ‘damu salama’
kufanikisha zoezi la uchangiaji damu, ambaye wanatarajia kufanya tena ndani ya mwezi
huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...