Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
KIONGOZI
wa mbio za mwenge maalum wa uhuru, LT.Josephine Mwambashi amekemea
vitendo vya baadhi ya watu wanaoharibu miundombinu ya maji ,ambapo
ameiasa jamii kulinda na kutunza vyanzo na miundombinu ya miradi ya
maji.
Akizindua
mradi wa maji Kijiji cha Nyaminywili , Rufiji mkoani Pwani,unaosimamiwa
na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) na kukamilika
kwa asilimia 100 kwa gharama ya milioni 195.358.2, Mwambashi alisema,
maji ni uhai yapaswa kulinda miundombinu yake kwa manufaa ya jamii.
Alisema,
serikali ya awamu sita ,inayoongozwa na Rais Samia Suluhu inajitahidi
ili kila mwananchi afikiwe na huduma muhimu ikiwemo maji.
Mwambashi
alifafanua, serikali imejipanga kwa kutenga fedha kutekeleza miradi ya
maji ,mijini na vijijini ili kuondoa tatizo sugu la maji kwa kumtua ndoo
mama kichwani.
"Wasimamizi
wa miradi hii inapaswa nanyi muwe wazalendo na kuwashirikisha wananchi
katika hatua za utekelezaji"alibainisha Mwambashi.
Hata
hivyo , Mwambashi alielekeza RUWASA kuandaa taarifa ya kiasi cha
sh.milioni mbili ambazo hazijawekwa katika taarifa ya mradi huo .
Awali
akielezea,mradi huo ,meneja wa RUWASA Rufiji,Tluway Ninga alisema,
makisio ya mradi huo yalikuwa milioni 257.543.3 , utekelezaji ulianza
julai 2020 na kukamilika julai 2021.
Ninga
alisema kuwa, mradi huo unasaidia wakazi 2,573 wa Nyaminywili kwa
kupata huduma ya maji safi na salama na kuondokana na kero hiyo sugu
iliyodumu kwa miaka takriban 30.
Mkuu
wa wilaya ya Rufiji,Meja Edward Gowelle alisema ,amepokea mwenge maalum
wa uhuru agost 14 mwaka huu ukitokea Wilayani Kisarawe.
Meja Gowelle alielezea kwamba ,miradi sita itatembelewa na mbio za mwenge huo ,miradi yenye thamani ya sh.milioni 500.8 .
Mwenge
ukiwa Rufiji pia umeweka jiwe la msingi katika ghala la mazao ya Kijiji
cha Ndundunyikanza ,ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Ujamaa
huko Ngorongo ,jiwe la msingi jengo la OPD zahanati ya Kijiji cha
Mkongo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...