Na John Walter-Manyara.

Taasisi za serikali,binafsi,Wadau wa Maendeleo na wenye mapenzi mema wametakiwa kuwa na utaratibu wa kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii wakiwemo wenye ulemavu wa aina mbalimbali.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi na mwanzilishi wa kituo cha Zilper Foundation chenye makao makuu mtaa wa Hangoni Mjini Babati katika mkoa wa Manyara Letion Marai amesema lengo la kituo ni kuhakikisha katika jamii pasiwepo mtoto mwenye ulemavu ambaye hatapata huduma.

Marai amesema Zilper wanawapokea watoto wenye matatizo yanayohitaji upasuaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania ambapo wanatumia watendaji katika mitaa au vijiji kuwapata.
Amesema wana mfadhili mmoja ambaye anagharamikia gharama za upasuaji katika hospitali zenye madaktari bingwa Seliani na KCMC, ambapo kwa kila mwezi anajitolea kuwadumia watoto tisa kupata upasuaji lakini changamoto inayowakabili ni ukosefu wa wafadhili wa kusaidia mahitaji mbalimbali kwa watoto ambao wapo kituoni wakisubiri kupatiwa matibabu Kwani wengi wao wanatokea katika mikoa ya mbali.

Msaada unaohitajika ni chakula,lishe na mahitaji mengine ya watoto.
Amesema kwa mwaka 2021 wameshapokea watoto 93 ambao wengi wao wameshahudumiwa na kuruhusiwa kurejea majumbani mwao na waliobaki kituoni ni 15 ambao nao wanasubiri muda wa kwenda Kwenye matibabu.

Anna msafiri ni mwanafunzi wa darasa la tano kutoka Dodoma alikuwa na mguu mmoja, anasema baada ya kufika kituoni hapo amehudumiwa kwa kupatiwa mguu wa bandia na sasa anaweza kutembea na matarajio yake ni kuendelea na masomo.

'Asubuhi nawapikia chai, chakula cha mchana,kuwaogesha na kuwafulia nguo zao lakini changamoto ni kwamba Kuna wakati mahitaji yanakosekana kutokana na kukosa wadau wa kutoa misaada' alieleza Mlezi wa watoto katika kituo hicho Elizabeth Samweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...