Mwenge wa Uhuru umekagua, kuona , kuzindua na kuweka mawe ya msingi wa Ujenzi wa miradi 13 yenye thamani ya shilingi 1.8 katika Wilaya ya Tandahima.

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa  zahanati ya Kijiji cha Miuta, mradi wa  TEHMA katika hospital ya Wilaya,  ujenzi wa tawi la benki ya wananchi wa Zanzibar,  ujenzi wa Kiwanda cha Korosho cha JABARI, na ujenzi wa nyumba nne za walimu shule ya Msingi Kuchele.

Katika hatua nyingine Mwenge huo  wa Uhuru umetoa siku saba kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoani Mtwara kuwasilisha nyaraka za uendelevu wa mradi wa maji wa Makonde uliopo katika Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi alitoa agizo hilo mara baada ya kutembelea kuona na kukagua uendelevu wa Mradi huo wa Makonde ambao umegharimu shilingi milioni 162.5.

Mradi huo ulizinduliwa na mbio za Mwenge Kitaifa 2019 lakini umeshindwa kuendelezwa kama ilivyokusudiwa kwa kujenga mabomba manane kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi.

“Mwenge wa Uhuru unatoa mda wa wiki moja kwa RUWASA mkoa, popote pale mwenge huu utakapokuwa upate taarifa za uendelevu wa mradi huo,” amesema.

Pia Mwenge huo umewataka RUWASA  kufanya matengenezo ya miundombinu ya pampu ya chanzo cha maji cha mradi huo na kuweka dawa  kwenye maji ya tenki la kuhifadhi maji yanayotumiwa na wananchi wa eneo Hilo ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Luteni Mwambashi amesema kwa mda mrefu wananchi wamekuwa wakinywa maji ambayo hayajatibiwa kwa mda mrefu, huku akilaumu wasimamizi wa mradi kutokuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu yao.

Kufuatia hatua hiyo, Luteni Mwambashi alimuomba Mkuu wa Wilaya Kanali Patric Sawala kusimamia na kuhakikisha miundombinu ya pampu katika chanzo cha maji inafanyiwa matengenezo na kutibu maji kwenye tenki la maji ili wananchi wapate maji safi na salama.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya (kulia) tayari kuukimbiza katika Wilaya ya Tandahimba

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi (anayenyoosha mkono) akiwa katika moja ya kibanda cha maji cha mradi wa maji wa Makonde Wilaya ya Tandahimba ambapo alifika kukagua kibanda hicho kuona kama maji yanatoka.
Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 akiwa amepanda juu Tenki la maji yanayotumiwa na wananchi wa Tandahimba Mjini Kwa ajili ya kukagua ubora wa maji na kuona kama kuna vifaa na dawa ya kutibu maji ambapo hata hivyo havikuwepo. Waliosimama ni viongozi wa Wilaya na wasimamizi wa mradi wa maji wa Makonde (RUWASA) pamoja na kiongozi wa Mwenge Luten Mwambashi aliyefika eneo Hilo kukagua mradi huo wa maji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi (kulia) akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tandahimba Mjini mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa maji wa Makonde uliyopo katika Tandahimba Mjini. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...