Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubongo Bi, Beatrice Dominuo akikabidhi hati ya kibali cha utekelezaji wa mradi wa hati yangu maisha yangu katika wilaya ya Ubungo wakati wa uzinduzi wa mradi huu wenye lengo la kuwawezesha wanawake kupatiwa hati miliki ya ardhi zao na elimu ya sheria za ardhi ili kuwawezesha wanawake kiuchumi. Mradi wa hati yangu maisha yangu unafadhiliwa na Legal Services Facility – LSF na kuendeshwa na chama cha wanasheria wanawake Tanzania TAWLA. Akishuhudia Mary Richard, Mkuu wa program TAWLA.
Na Mwandishi wetu
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Legal Service Facility LSF kwa kushirikiana na chama cha wanasheria wanawake Tanzania TAWLA pamoja na halmashauri ya wilaya ya ubungo wamezindua mradi utakaowawezesha wanawake wanaomiliki sehemu ya ardhi katika wilaya ya ubungo kupata hati za umiliki wa Ardhi.
Afisa mtendaji mkuu was LSF Lulu Ng'wanakilala amesema mradi huo umeanzishwa ili kukabiliana na changamoto zinazowakumba wanawake wa hali ya chini ambao wanamiliki ardhi lakini wameshindwa kukamilisha zoezi LA umilikidhwaji kutokana na kutoweza kumudu gharama za upatikanaji wa Hati.
"Tunayofuraha kubwa kubuni mradi huu na kutoa ruzuku kwa TAWLA kutekelezwa kwa lengo LA kuboresha maisha ya wanawake na kusaidia kupunguza umaskini" Alisema lulu.
Bi lulu ameongeza kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanapitia changamoto nyingi zikiwemo unyanyasaji wa kijinsia,kutopata fursa saws katika masuala ya kiuchumi ,kiuongozi lakini pia wamekuwa na majuku mazito katika kulea na kuhakikidha ustawi wa familia zao unakwenda vizuri.
"Kupitia mradi huu tutaweza kuwafikia wanawake 2000 kwa kuwapatia rlimu na zaidi ya wanawake 3000 watapata hati miliki zao kwa kuchangia gharama kidogo sana na hii ni nafasi ya kipekee kwa wanawake wanaoishi katika wilaya ya ubungo kunufaika kwa kuchangamkia fursa hii "
"Mradi huu pia umelenga kutoa elimu kwa wanachi huu ya sheria ya kurithi na kumiliki ardhi ili kuongeza uelewa na kupunguza changamoto zinazowaathiri wanawake kwa sasa " Alisema Lulu.
kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo Bi, Beatrice Kwai ametoa shukrani za dhati kwa TAWLA ambao ni watekelezaji wa programu hiyo pamoja na LSF ambao ni wafadhili , kwa kuweza kutambua changamoto zinazoikumba wilaya ya ubungo.
Mradi huo ujulikanao kama "Hati yangu maisha yangu" umezinduliwa katika wilaya ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya majaribio lakini lengo ni kuutekeleza programu hiyo nchi nzima na Ili kunufaika na mradi huu wanawake kutoka katika kata za Mbezi, Goba, Kwembe, Kibamba na Msigani watatakiwa kushiriki wakati wa zoezi zima litakapoanza, zoezi hili litawalenga wanawake wenye uwezo mdogo ambao wanamiliki vipande vya ardhi lakini wameshindwa kupata hatamiliki kwasababu ya gharama za upatikanaji wa hatimiliki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...