Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jamii imetakiwa kujenga utamaduni wa kuwa tembelea wafungwa na kutoa misaada ya hali na mali katika magereza mbalimbali hapa nchini kufuatia wafungwa kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na kukosa mahitaji mhimu .
Wito huo umetolewa na familia ya Philipo Filikunjombe ya wilayani Ludewa ilipotembelea katika gereza la Ibihi wilayani humo na kutoa misaada ambayo wafungwa waliomba katika sikukuu ya Iddi mwezi may mwaka huu mara baada ya chakula cha pamoja.
“Cha kwanza ilikuwa huduma ya dawa amabayo tumeleta,waliomba TV ya nchi 50 tumeshaileta na waliomba yebo pisi 250 nazo tumezileta na sisi kwa niaba ya familia tuliguswa kwasababu hawa ni wenzetu”alisema Vestina Chaula mwanafamilia ya Filikunjombe
Mara baada ya kupokea misaada hiyo mkuu wa gereza la Ibihi sp joannnes baitange amesema kuwa wafungwa wanamahitaji mengi na kuwa msaada huo wa viatu vya kuogea maarufu yebo , runinga na huduma ya kwanza vitasaidia kuimarisha afya zao.
“Tunawashukuru sana kwa moyo wa kujitoa na tunaomba mwenyezi Mungu aweze kuwarejeshea palio mliovitoa “ alisema Joannnes Baitange mkuu wa gereza Ibihi Ludewa
Familia hiyo imetoa msaada wa vitu vya thamani ya shilingi million 4 na laki 7 ambapo wafungwa watapata fursa pia ya kupata taarifa kupitia runinga waliyokabidhiwa.
Baadhi ya maafisa wa jeshi la magereza wakipokea TV ya nchi 50 iliyotolewa na familia ya Filikunjombe kwa ajili ya wafungwa.
Baadhi ya maafisa wa magereza wakipokea yebo kwa ajili ya wafungwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...