Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amevielekeza vyombo vya dola kumkamata Mkurugenzi wa Kampuni ya Upimaji wa Ardhi ya Geolink Solution Tanzania LTD kwa tuhuma za kukusanya fedha za Wananchi zaidi ya Shilingi Milioni 18 wa eneo la Mtaa wa Mbezi Kati kwaajili ya zoezi la Upimaji wa Ardhi na kuingia mitini.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kusikiliza Migogoro Jimbo la Kawe ambapo ameelekeza pia kampuni zote zilizochukuwa fedha za Wananchi na kuingia mitini wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kero ya Wananchi hao zaidi ya 100 wa eneo la Maendeleo mtaa wa Mbezi Kati limeibuliwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo aliejumikana kwa majina ya Frank Mwanga.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...