Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wanawake wilayani Makete mkoani Njombe wanakabiliwa na changamoto kubwa ya malezi kwa watoto kutokana na wanaume kutelekeza familia zao kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo maswala ya uchumi.

Aidha ukatili wa utelekezaji wa watoto unatajwa kukithiri wilayani humo kutokana na akina baba kukimbia familia zao huku pia wanawake wengine wakizaa watoto mijini na kuwatekeleza kwa bibi zao vijijini.

Hayo yamebainishwa na Bi,Ester Ramosai afisa wa maendeleo ya jamii wilaya ya Makete ambaye ni mratibu wa shughuli za kudhibiti UKIMWI wilayani humo na mjumbe wa kamati ya kutokomeza unyanyasaji na ukatili kwenye kamati ya mwanamke na motto alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano wa jukwaa la amoja na wananchi wa kijiji cha Usagatikwa kata ya Tandala wilayani humo.

“Maswala ya ukatili na unyanyasaji yapo juu na kuna matukio mengi ambayo yanaripotiwa kwenye ofisi ya ustawi wa jamii na ukatili ambao unaongoza ni ukatili wa utelekezaji kwa kuwa wanaume ndio wanao kuwa wa kwanza kukimbia watoto”alisema Ester Ramosai

Pia ameongeza kuwa wanawake wamekuwa wakizaa watoto huku wakiwa mjini na kuwapeleka vijijini wakilelewa na wazee hatua inayosababisha watoto kukosa usimamizi na kusababisha matukio ya ubakaji na wengine wakishindwa kuhudhuria shuleni kwa kukosa mahitaji.

Aidha amesema serikali inaendelea kujenga mifumo imara itakayokuwa chachu ya kudhibiti maswala ya ukatili wa kijinzsi kwa kutoa elimu na kusimamia sheria kwa wote watakao sababisha maswala ya ukatili.

Suzan Kawanga ni wakili kutoka shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika (WiLDAF) ambao ni watekelezaji wa mradi wa mwanamke imara unaofadhiliwa na watu wa Marekani,amesema lengo lao ni kuhakikisha wanapinga ukatili dhidi ya wanawake na vijana amesema wamebaini kuwepo kwa vipigo dhidi ya wanawake katika kijiji hicho hatua inayowalazimu kuwekeza nguvu ya kutoa elimu ili kudhibiti vitendo hivyo.

“Tumejifunza kuwa eneo hili kuna vipigo sana dhidi ya wanawake lakini pia hata wanaume wanafanyiwa ukatili na wanaume wengi wanatelekeza familia zao.Kwa hiyo lengo letu ilikuwa ni kujifunza ukatili gani upo sana na tufundishane namna ya kudhibiti tunashukuru tumefanikiwa kwa hilo”alisema Suzan Kawanga

Petro Sigala na Jema Nyaluke ni miongoni mwa wananchi wa kijiji cha Usagatikwa wamekiri kuwepo kwa ukatili mbali mbali ukiwemo wa kupigana pamoja na kupiga watoto katika kijiji chao na kusababisha matatizo makubwa ndani ya jamii.

“Kweli ukatili upon a hapa upo wa kupigana pamoja na kupiga watoto kwa hiyo elimu tuliyoewa haa leo ni nzuri sana na tunaamini tutaenda kujirekebisha kwasababu kila mmoja emefurahia elimu ya leo”alisema etro Sigala

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wakili kutoka shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika (WiLDAF) amesema shirika hilo kwa sasa katika mkoa wa Njombe linafanya kazi katika wilaya mbili za Makete na Ludewa kwa kupita kata tano kwenye kila wilaya na kufanya shughuli mbali mbali zinazoambatana na kutoa elimu pamoja na kupinga maswala ya ukatili wa kijinsia.

Suzan Kawanga wakili kutoka shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika (WiLDAF) akitoa elimu dhidi ya ukatili  kwa wananchi wa kijiji cha Usagatikwa mara baada ya kufika kijijini hapo na kutambua aina ya ukatili unaofanyika kijijini hapo.

Baadhi ya wananchi wakipewa elimu ya kumlinda mototo kwa mfano anuai uliokuwa ukitolewa na mmoja wa watoa mada katika mdahalo huo wa pamoja na wananchi wa kijiji cha Usagatikwa.


:Waananchi wa kijiji cha Usagatikwa kata ya Tandala wilayani Makete wakiwasikiliza wawezeshaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...